Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haya maswala ya takwimu wangeachana nayo tuu kwa sababu kuna watu kuwaambia kwamba Pato lao kwa mwaka ni m3+ ni kebehi na matusi unakua umeamua kuwatukana tuu, maskini wanazidi kua maskini kila siku alafu unawaambia eti pato lao limeongezeka si utani huuu
Kilq mtu ana haki ya kula.. Aliyesoma ma aaoyesoma.. Tajiri na maskini.. Mtakapowqbana sana maskini na wasiosoma mpaka wakakosa mlo wao kwa sababu ya ulafi wenu ipo aiku hamtaamini watakachowafanya..Km hujaenda shule jilaumu kwa uzembe wako
Uongo mtupu nyambaf kabisaNapata hasira sana nikisikia taarifa za namna hii!
Jaribu kuficha upumbavu wako sio lazima kila mmoja ajue wewe ni mpumbavuNenda shule ujinga wako usiwe mzigo kwa wengine
Mshahara wangu ni 327,000/= Ninakatwa mkopo 122,500/=. Take home baada ya makato na michango 154,415/=Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi, amesema Tanzania imeendelea kuwa katika kundi la Nchi zenye uchumi wa pato la kati, ikimaanisha pato la wastani la kila Mwanachi kwa mwaka (GNI per capital) ambapo mwaka 2019 ilikuwa dola 1,080 (Tsh. 2,743,813) lakini kwa mwaka 2022 ni dola 1,200 ( Tsh. 3,048,681).
Akiongea Jijini Dar es salaam leo, Matinyi amesema “Uchumi wa Tanzania umeendelea kukua licha ya athari kubwa za mlipuko wa UVIKO-19 duniani pamoja na vita za Urusi na Ukraine na pia huko Mashariki ya Kati, matatizo haya yaliutikisa uchumi wa Tanzania uliokuwa umefikia wastani wa ukuaji wa zaidi ya 7% na kuushusha hadi 4.2% mwaka 2020”
“Hata hivyo, hivi sasa ukuaji umefikia 5.2% kutokana na uongozi thabiti wa Serikali ya awamu ya sita ambapo Tanzania imeendelea kuwa katika kundi la Nchi zenye uchumi wa pato la kati, ikimaanisha pato la wastani la kila Mwanachi kwa mwaka (GNI per capital) ambapo mwaka 2019 ilikuwa dola 1,080 (Tsh. 2,743,813) lakini mwaka 2022 ni dola 1,200 ( Tsh. 3,048,681)”
“Serikali pia imeendelea kudhibiti mfumuko wa bei ambapo kwa sasa ni chini ya 4% - kiwango ambacho ni miongoni mwa viwango bora katika nchi za jumuiya za kikanda ambazo Tanzania ni mwanachama, kama Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)”
“Akiba ya fedha za kigeni imeendelea kuwa toshelezi ambapo katika kipindi chote cha miaka mitatu hadi December 2023, Nchi ilikuwa na akiba inayotosha kuagiza bidhaa kutoka nje ya Nchi kwa miezi 4.5, ikiwa ni kiwango cha juu ya lengo la miezi 4, akiba hiyo ni sawa na dola za Marekani bilioni 5.4”
Duh noma mkopo wa bank au board ya mkopo?Mshahara wangu ni 327,000/= Ninakatwa mkopo 122,500/=. Take home baada ya makato na michango 154,415/=
154,415 X 12 = 1,852,980/=.
Wenzangu mna siri sana. Yaani mnachukua mara mbili ya ninachokipata kwa mwaka. Daaaah