Msemaji wa Azam anashangaza sana! Anahisi ushindi wa Azam kuna mkono wa Simba!

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Nimeona video clip ya msemaji wa Azam akilalamikia ushauri wa Simba kwa Azam kwamba washinde mechi yao dhidi ya Yanga.

Jambo hilo halikumfurahisha kiasi kwamba amefikia kuhoji kwamba Simba inaweza kuwa imehusika kupanga matokeo?

Kusema kweli malalamiko hayo nilidhani yalipaswa kutolewa na waliopoteza mechi yao. Mchezo walicheza wao, kufunga walifunga wao, kwa nini aje kulalamikia Simba?

Simba ina CEO mmoja tu, je aliwaandikia barua Azam washinde? Mbona huyu jamaa simuelewi kabisa?

Hana furaha kwa Azam kushinda? Sasa kwa nini hakuwaambia wachezaji wake wasishinde mechi? Atakuwa na furaha na Dube kweli huyu? Hivi Azam mnaajiri vipi mtu huyu anaonekana hawezi kabisa kuficha hisia zake za mapenzi na club ya yanga? Hivi mmekosa kabisa watu wanaoweza kuficha unazi wao kwa timu hizi kongwe?
 
😂😂😂 yani mtu anawatakia mema yeye ana kasirika au anawakoga vyura wazidi kuichukia simba.

Uyujamaa anazingua tu, utopo wao wapokee kipigo kama kipigo kutoka kwa Azam.
 
Nadhani ujamuelewa Zakazakazi ebu isikilize vizuri hiyo clip hoja ni kwamba Azam inataka isilazimishwe na influence Simba kushinda game waache wenyewe washinde game zao.
 
Nadhani ujamuelewa Zakazakazi ebu isikilize vizuri hiyo clip hoja ni kwamba Azam inataka isilazimishwe na influence Simba kushinda game waache wenyewe washinde game zao.
Pengine yupo sahihi lkn sura yake haioneshi furaha hata kidogo kwa hiyo hilo limemuuzi kiasi ambacho
 
Sikiliza clip kwa umaakini. Unachoelezea sicho.

Kwa kifupi, anasema wao Azam hawahitaji kuambiwa washinde mechi na Simba au timu yoyote. Wanajua wajibu wao.

Ni sawasawa wote mumeoa ila kaka yako anakupangia cha kufanya kwenye ndoa yako.
 
View attachment 1764366

Paw pandisha hii clip kwenye uzi. Huyu Zaka ni Yanga, kimeemuuma sisi kui push Azam
Hili jamaa.ni utopolo ushindi wa jana umemuuma na ndio wanaifanya Azam isisonge mbele, siku Azam wakicheza na yanga ni wazi Azam wataomba Simba iwafunge yanga ili wao washike nafasi ya pili limetoa poor reasoning
 
Sikiliza clip kwa umaakini. Unachoelezea sicho.

Kwa kifupi, anasema wao Azam hawahitaji kuambiwa washinde mechi na Simba au timu yoyote. Wanajua wajibu wao.

Ni sawasawa wote mumeoa ila kaka yako anakupangia cha kufanya kwenye ndoa yako.
kulikuwa na haja ya povu lote hilo?mbona issue ni petty sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…