Msemaji wa Jeshi la Polisi ashambuliwa na raia kwenye mazishi ya ASP Kirumira

Msemaji wa Jeshi la Polisi ashambuliwa na raia kwenye mazishi ya ASP Kirumira

COARTEM

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2013
Posts
3,603
Reaction score
3,658
Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda Emilian Kayima, Ameshambuliwa kwa mawe na raia wenye hasira kali wakati akizungumza na wanachi katika Mazishi ya aliyekuwa askari polisi Muhammed Kirumira aliyekufa kwa kupigwa risasi Usiku wa kuamkia jana Bulenga.

Hata hivyo katika Hotuba yake, Msemaji huyo amevilaumu vyombo vya ulinzi na usalama nchini humo kuhusika na tukio hilo siku ya jumamosi ya tarehe 8/9/18 usiku katika wilaya ya wakiso, Vile vile kabla ya kifo chake, Marehemu Mohhamed Kirumira alikuwa ni mkosoaji mkubwa wa uvunjifu wa haki za raia na kiongozi wa jeshi la polisi nchini humo Kale Kayihura.
Bobi Wine: Kirumira was assassinated
 
ivi na polisi wa uganda ni wale wenye leaving cert. tu kama wetu hawa.
 
Ila nao wana moyo wa chuma unaanzaje kwenda kwa mfano

FB_IMG_1536510416657.jpg
 
Hadi huruma inasikitisha sana,bora ukutane na mnyama ila sio binadamu.
 
NACHAGUA KUISHI ACHA WABAKI NA SIASA ZAO WALAHI!
Rip
 
Hadi huruma inasikitisha sana,bora ukutane na mnyama ila sio binadamu.
Ogaaah! Halafu huyo M7 akumbuke yy mwenyewe ndye aliyekuwa akipambania utawala dhalimu wa IDD AMIN nashangaa ameurudsha
Mwaka 1975 Aboud Jumbe,Rais wa Zanzibar aliwahi kuja mahali fulanibmkoa wa Pwani, na nakumbuka alichosema, "Makaburu nao risasi zinawapenya".
M7 asisahau, naye risasi zitampenya.
 
Ogaaah! Jamani M7 alishasema hafanyi kazi kwa ajili ya watu Bali anafanya kazi kwa ajili ya watoto wake na wajukuu zake
 
Huyu jamaa kwa hiyo alizikwa na waislamu pekee?vichwa vya habar vingine ni vya kichochezi!ha ha
 
Back
Top Bottom