Blessed Tajiri
JF-Expert Member
- Dec 16, 2023
- 284
- 870
Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa anazungumza na waandishi wa habari leo Juni 11, 2025 saa saba na nusu mchana..... ngoja tusubiri kusikia boko litakalotoka kwa serikali leo... Rais alijishikilia kweli juzi na jana, leo watakuwa wanaangusha bomu.
===========================
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amewaonya Vijana wanaoandika habari za uchochezi mitandaoni, zinazodhalilisha Watu na kuzua taharuki, kuacha mara moja kufanya hivyo akisema Serikali ina mkono mrefu na itawapata tu Vijana hao na kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo faini ya zaid ya Tsh. milioni 5 na kifungo cha miaka mitatu au vyote kwa pamoja.
Akiongea Jijini Dodoma leo June 11,2025, Msigwa amesema ““Wakati mwingine unaona vikampeni havina mbele wala nyuma nikisema wanasema Msigwa ametusemea maneno makali lakini nachosema Vijana tutumie mitandao kwa njia za kimanufaa, ukifanya makosa tutakupata”
“Sheria inakataza kutukana, kufanya uchochezi, kudhalilisha na kuzua taharuki, tumeanza kuona kwenye mitandao Watu wanafanya makosa hayo, naomba niwaambie Vijana hakuna atakayefanya makosa hayo akabaki salama tutakupata tu itakuwa ni suala la muda tu hatukukupata leo tutakupata kesho, keshokutwa, Wiki ijayo au mwakani jinai haifi”
“Na tukiwakamata Vijana hawa wengi utasikia nilikuwa sijui, kutokujua sheria sio kinga ukifanya makosa ya mtandao uwe unajua au haujui sheria ni msumeno, kifungu cha 16 kinasema wazi umeandika habari za uchochezi, za kuzua taharuki, za kudhalilisha Watu, tukikupata na ukithibitika na Mahakama faini milioni 5 au zaidi, kifungo kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja”