Msemaji wa Serikali, huoni umuhimu wa kuwa na account hapa JamiiForums?

Msemaji wa Serikali, huoni umuhimu wa kuwa na account hapa JamiiForums?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,828
Reaction score
165,667
Ndugu kiongozi,kama unaweza kuwa na account twitter na kwenye mitanda msingine,ni kwanini huoni umuhimu wa kuwa na account hapa JamiiForums ili muweze kujibu na kutolea ufafanunuzi wa mambo mbalimbali yanayoihusu serikali na pia Kuitumia account hiyo kutolea taarifa za mambo mbalimbali yanayoihusu serikali?

Kama wafuasi na watetezi wa chama na serikali wanaitumia JamiiForums kwa mambo mbalimbali ya kutetea chama na serikali,kwanini ofisi yako haioni umuhimu huo?

Natoa wito pia kwa vyama vya siasa kama vile CHADEMA,ACT-Wazalendo,CCM na vyama vingine vifungue account hapa JamiiForums kwani mtandao huu hauna upande wowote katika siasa za nchi hii na ni pia unatumika sana na wafuasi na washabiki wa vyama hivi vya siasa sambamba na wale wasio na vyama.

Jifunzeni kwa Zitto jinsi anavyoitumia JamiiForums sambamba na mitandao mingine(mwanasiasa kinara katika matumizi ya mtandao kwa mtazamo wangu).

Huwa nashangaa sana watu wanapolaumu huu mtandao ila hali hata wao wako huru kujinga na kuja kujibu hoja zinazowahusu.na pia kuanzisha hoja/mada kama watumiaji wengine.
 
 
Atasababisha watu wengi wapigwe ban sababu majibu ya serikali hii ya awamu ya tano yanatia kinyaa.
 
Wazo zuri
Lakini kabla ya kuanzisha uzi humu ni vizuri ukatafuta kuona kama mada ilishajadiliwa


Hii content ilishaletwa hapa
 
Mpigie simu Mbowe umwambie kufungua akaunti ni bure!
 
Hao wote wana account humu lakini sio verified. Ni vyema wakaja na verified account ili wakutane na maoni halisi na sio hayo yaliyoratibiwa.
 
Hao wote wana account humu lakini sio verified. Ni vyema wakaja na verified account ili wakutane na maoni halisi na sio hayo yaliyoratibiwa.
Alafu kama ni lugha zisizo na staha,mbona hata huko twitter,facebook,instagram na kwingineko lugha hizo zipo?
 
Back
Top Bottom