GE2025 Msemaji wa Serikali: Madai kwamba uhuru wa kisiasa umepungua kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 siyo ya kweli

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Serikali imekanusha madai yanayodai ongezeko la ukandamizaji wa kisiasa nchini humo, huku taifa likielekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akijibu ripoti iliyotolewa na Shirika la Kutetea Haki za Binadamu, Human Rights Watch (HRW), Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema madai hayo hayana msingi na yanapotosha hali halisi ya nchi.

“Madai kwamba uhuru wa kisiasa umepungua kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 siyo ya kweli,” amesema Msigwa. Amesisitiza kwamba katiba ya Tanzania inatoa haki ya kuishi, usalama na uhuru kwa kila Mtanzania.

Aidha, Msemaji huyo amepuuzilia mbali madai ya taarifa za kutekwa kwa raia nchini humo na kulaumu shirika la HRW kwa kutoa ripoti hiyo bila kuipa serikali fursa ya kujibu. Hata hivyo, amesema serikali ipo tayari kushirikiana na taasisi yoyote inayohitaji taarifa sahihi.

Kwa mujibu wa ripoti ya HRW, Serikali ya Tanzania imedaiwa kukandamiza upinzani, kunyamazisha vyombo vya habari na kushindwa kuhakikisha uhuru wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Ripoti hiyo pia inatoa wito kwa mamlaka kuchukua hatua za haraka kulinda uadilifu wa uchaguzi mkuu, ambao shirika hilo linasema uko katika hatari.

Nomathamsanqa Masiko-Mpaka, mtafiti wa Afrika katika HRW, amesema:
“Mamlaka inahitajika kujizuia kukandamiza upinzani na vyombo vya habari, na badala yake kushiriki katika mageuzi yenye maana ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, wa haki na wa kuaminika.”

Serikali ya Tanzania imefafanua kwamba imejipanga kuhakikisha haki za binadamu, demokrasia, utawala bora na heshima ya sheria vinazingatiwa kabla, wakati, na baada ya uchaguzi mkuu wa 2025.
 
Maelekezo Maalum kuhusu tarehe 29 Oktoba.

Siku hiyo kazi ni rahisi sana

Viongozi wa CCM tunaishi nao mitaani; Nyumba zao zipo mitaani kwetu, mali zao zipo mitaani kwetu.

Ofisi za CCM zipo mitaani kwetu. Ofisi za Umma nazo zipo mitaani kwetu

VItuo vya kupigia kura vipo mitaani kwetu

Mawaziri, Wabunge na Madiwani tunaishi nao mitaani kwetu, familia zao na ndugu zao tunaishi nao mitaani kwetu

Tukafanye kazi iliyotukuka hiyo Oktoba 29 hadi hawa Mafisadi watuheshimu na wakome kutuchezea na kutuua.

Share na mwenzako
 
Kwa sasa ana haki ya kujibu kisiasa hayo maswali. Ila muda ukifika wa watu kudai haki zao za msingi, ndiyo atajua kumbe upotoshaji na porojo siyo vitu vizuri katika nchi.
 
Serikali imekanusha madai yanayodai ongezeko la ukandamizaji wa kisiasa nchini humo, huku taifa likielekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akijibu ripoti iliyotolewa na Shirika la Kutetea Haki za Binadamu, Human Rights Watch (HRW), Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema madai hayo hayana msingi na yanapotosha hali halisi ya nchi.

“Madai kwamba uhuru wa kisiasa umepungua kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 siyo ya kweli,” amesema Msigwa. Amesisitiza kwamba katiba ya Tanzania inatoa haki ya kuishi, usalama na uhuru kwa kila Mtanzania.

Aidha, Msemaji huyo amepuuzilia mbali madai ya taarifa za kutekwa kwa raia nchini humo na kulaumu shirika la HRW kwa kutoa ripoti hiyo bila kuipa serikali fursa ya kujibu. Hata hivyo, amesema serikali ipo tayari kushirikiana na taasisi yoyote inayohitaji taarifa sahihi.

Kwa mujibu wa ripoti ya HRW, Serikali ya Tanzania imedaiwa kukandamiza upinzani, kunyamazisha vyombo vya habari na kushindwa kuhakikisha uhuru wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Ripoti hiyo pia inatoa wito kwa mamlaka kuchukua hatua za haraka kulinda uadilifu wa uchaguzi mkuu, ambao shirika hilo linasema uko katika hatari.

Nomathamsanqa Masiko-Mpaka, mtafiti wa Afrika katika HRW, amesema:
“Mamlaka inahitajika kujizuia kukandamiza upinzani na vyombo vya habari, na badala yake kushiriki katika mageuzi yenye maana ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, wa haki na wa kuaminika.”

Serikali ya Tanzania imefafanua kwamba imejipanga kuhakikisha haki za binadamu, demokrasia, utawala bora na heshima ya sheria vinazingatiwa kabla, wakati, na baada ya uchaguzi mkuu wa 2025.

Mbona hawako settled kabisa. Nchi wanayo wao, wasiwasi wa nini?
 
Tarehe 29 tukiikomboa nchi huyu Msigwa apigwe kama ngoma
 
Kwa sasa Tanzania yawezekana ni nchi inayoongoza katika kugandamiza haki za binadamu Duniani. Hakuna nchi Duniani kwa sasa ambayo utekaji na mauaji ya wakosoaji, vimeshamiri kwa kiwango cha kutisha, kama Tanzania.
 
Back
Top Bottom