Msemaji wa serikali: Uchumi wa Tanzania umekua kwa 6.9%

Msemaji wa serikali: Uchumi wa Tanzania umekua kwa 6.9%

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema kwa takwimu za mpaka September 2019, uchumi wa Tanzania umekua kwa 6.9% huku matarajio yakiwa ni kufikia hadi 7.1% “kwa Afrika Mashariki tunahangaika na Rwanda, kwa Nchi za SADC Tanzania ni miongoni mwa Nchi ambazo zinaongoza kwa uchumi wake kukua kwa kasi" .

"Uchumi unaokua unaweza kuupima kwa namna nyingi mojawapo ni maisha ya Watu, Tanzania ukienda Shule elimu bure, angani kazi zinafanyika, vyuo vikuu ada Wau wanalipiwa, kuakisi kwa uchumi kukua maana yake ni uwezo wa Serikali kufanya mambo mengi" - Dr. Abbas .

"Katika Ripoti ya Transparency 2019 ya January 23, 2020, Tanzania imekuwa ya 96 kutoka ya 117 mwaka 2015 na 103 mwaka 2017, kwa matokeo haya Tanzania ni ya pili kwa Afrika Mashariki kwa kutokuwa na rushwa nyuma ya Rwanda"- Dr. Abbas.
 
sawa
IMG_20200130_201414.jpg


Sent from my SM-J320H using JamiiForums mobile app
 
Nasikia maisha yamekuwa safi lakini wengine tunalia Hali ngumu 🤔🤔🤔🤔🤔🤔
 
Habari njema hii,lkn ukuaji huo u-reflect na maisha halisi ya mwananchi.

dodge
 
Hongera JPM, siku miundo mbinu unayojenga itaanza kufanya kazi, uchumi wa nchi utakua kwa "double digit".
 
Back
Top Bottom