Msemaji wa Simba Ahmed Ally akiri kupewa Mpinzani mgumu toka waanze kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa Afrika

Msemaji wa Simba Ahmed Ally akiri kupewa Mpinzani mgumu toka waanze kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa Afrika

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Meneja Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amefunguka baada ta droo ya robo fainali kumalizika na kupangwa kucheza dhidi ya Wydad Casablanca [emoji3596]

"Ni lazima tukiri kuwa tumepata mpinzani mgumu kwenye hatua ya robo fainali na pengine ni mpinzani mgumu zaidi tangu tuanze kushiriki hatua hii.

Hapa unamzungumzia bingwa mtetezi, unamzungumzia mshiriki wa Club World Cup, unazungumzia timu yenye wachezaji waliotoka nusu fainali ya Kombe la Dunia.

Huu ni mlima mrefu kwetu lakini hatuna budi kuupanda na kufika kileleni. Ili uwe mkubwa Afrika ni lazima uwafunge wakubwa wa bara hili.

Inawezekana sana Simba kupata ushindi dhidi ya Wydad kama tuu kila idara ndani ya taasisi yetu itatimiza wajibu wake kwa asilimia 100.

Kama tulivyomvua ubingwa Zamalek mwaka 2003 ni wakati sasa kumvua ubingwa Wydad.

Let’s go wana Lunyasi, Let’s goo wana Simba let’s wana Msimbazi mapambano yanaanza sasa,"

Source: Mwanaspoti

===

My take naona Ahmed anadhani wydad ni zamaleki na anashindwa kabisa kugundua mpira ule wa miaka hiyo ni tofauti kabisa na mpira wa kisasa.

Wacha tuone Nini kitatokea.
 
Najaribu kutulia ila hii picha inajirudia rudia kichwani.
Screenshot_20230213-073317_Twitter.jpg


Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Kasema ukweli, hao jamaa ni level nyingine isipokuwa kinachotakiwa kwa Simba Sc ni commitment ya 100% uwanjani kisha tusubiri matokeo.
 
Kasema ukweli, hao jamaa ni level nyingine isipokuwa kinachotakiwa kwa Simba Sc ni commitment ya 100% uwanjani kisha tusubiri matokeo.
Sasa wew umezungumza ukweli wako kabisa kutoka moyoni.
 
Back
Top Bottom