Msemaji wa Simba SC Ahmed Ally amepwaya sana katika nafasi yake

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Nimeona, nimemshuhudia na kumuona kutoka kila Angle na kufikia tamati kuwa Ahmed Ally amepwaya sana katika nafasi ile.

Yaani ukijaribu kumsikiliza kwa umakini unaona kabisa anajaribu kuforce kupita katika njia ile ya Haji Manara. Kiasi kwamba anaharibu hata identity yake ambayo amekuwa akijulikan anayo.

Hata ukimsikiliza kwa makini tena utagundua anamatamanio na mshawasha mkubwa wa kujitengenezea brand mpya tofauti na ile aliyo jijengea akiwa AZAM TV.

Nadhani Klabu ya simba ilikaa muda mrefu pasi na kuwa na msemaji/mkuu wa kitengo cha habari kutokana na kukosekana na mtu wa aina hiyo kwenye potential ya kuziba pengo la Manara na kufanya mashabiki wamsahau kabisa.

Ujio wake umekuwa wa lolote na liwe kwakuwa hata viongozi wanaonekana kumtenga kiaina fulani hivi kwa sababu wamemuona hana potential ya kuipa hadhi cheo kile.

Ataendelea kuwapo pale ili tu ile nafasi isiwe wazi.

Na sio kwasababu kazi yake inakidhi matakwa na mahitaji ya klabu kwa namna ambavyo Manara alikuwa akifanya.

Bela Ciao.
 
Tatizo lake anataka aongee kwa mbwembwe na mipasho- ingependeza akaongea Kama mtoa habari za timu bila mipasho wala mbwembwe nyingi.
 
Ana utoto mwingi labda akikua ataacha vumilieni tu
 
Uto mnavojipongeza.. mnajisahaulisha kuwa msimu wa mvua umeanza pilikapilika gongo wazi ndo zinaanza pale jangwani(krooooo!!! Krooooooo!!!!)
 
Manara mwenyewe umeamua kuja kujimwambafai.

Km huna shule kichwani huwezi kutofautisha kati ya Uafisa habari na mhamasishaji wa timu.

Ahmed Ally yule Ni professional ktk cheo alicho nacho, Ila we Zuzu/Utopolo Ni mpiga kelele, uko tayari hata kuvua nguo ili tu ndiyo uonekane unafanya kazi. Haina weledi.

Saizi yako Manara ni kina Mwijaku, wahamasishaji.
 
Kunahusiano gani mkuu kati ya Kupwaya kwake na mtokeo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…