blogger
JF-Expert Member
- Mar 13, 2012
- 12,112
- 15,060
Acha uchochezi..unahaha.Kama kuna Kitu ambacho GENTAMYCINE ninawapongeza Yanga SC kwani Wamekiweza na Kinawasaidia mno ni Kupenyeza Watu wao HATARI ndani ya Simba SC ( tena Jikoni kabisa ) halafu Waliopenyezwa nao kuwa Wasanii ( Waigizaji ) kwa kujifanya ni wana Simba SC na Wanaifia sana Timu kumbe nyuma ya Pazia wanatoa Ramani zote za Vita kwa Adui na Timu ikifungwa mbele ya Media wanajifanya Kuumia na Kusikitika ila wakiwa tu Mafichoni Kwao pale Gwambina ( zamani TCC Club Chang'ombe ) wanaanza Kucheka, Kukata Viuno na Misebene ya Kikongo huku Gari aina ya ALPHARD Nyeusi ya Ofisini kwa Tajiri Posta Juu Ghorofani ikileta Fedha kwa Kazi nzuri ya USALITI na KUTUUMIZA wana Simba SC huku Kinafiki / Kiunafiki ukijifanya uko pamoja nasi.
ANGALIZO
Huvutiwi na Taarifa / Habari zangu GENTAMYCINE hapa Jamiiforums njia ni rahisi tu achana na Mimi, usifungue Thread yangu na itapendeza zaidi kama utanibloku ( ignore ) ili tusichoshane na uniachie tu wale Werevu na Wanaonielewa na Kuniamini waendelee Kuhabarika kwa ninayoyaleta hapa ambayo kamwe huwezi kuyapata kwa yoyote yule.
Kuendelea kumsoma na kumfuatilia GENTAMYCINE ambaye kutwa HUMPENDI na HUVUTIWI na UWASILISHAJI wake na HUZIAMINI TAARIFA / HABARI zake kunaonyesha kuwa MOYONI mwako UNAMKUBALI ile mbaya
Nimemaliza.
Mimi ndiyo GENTAMYCINE The King!!!!!
Jipangeni mshinde next time...
Hisia haziwasaidii kitu..