Msemaji wa Simba unaanza kuharibu

Msemaji wa Simba unaanza kuharibu

Vikintu

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2021
Posts
2,051
Reaction score
3,162
Wapendwa nimemuona msemaji wa Simba huko YouTube akimtembelea na kumpongeza mzee aliyekuwa na kitochi uwanjani. Hii si sawa kwani anahamasisha vitendo vya utovu wa nidhamu unaoweza kuigharimu timu.

Kesho watu wakija na vitochi zaidi tena vyenye mwanga wenye madhara atafanyaje? Nilitegemea angekemea huo upuuzi lakini ndio kwanza ana uhamasisha.

Brother, wewe ni msemaji wa club kubwa, achana na vitu vya hovyo visivyo na tija.

NB: Niko tayari kwa povu.
 
Kama ni kweli hii siyo poa,

Mbona jamaa namuona Kama siyo mswahili
 
Duuh jamaa basickazingua.

Ule mwanga wa tochi ya mzee wala haukua na madhara kabisa ila kama sasa kaanza kutoa na hivyo vizawadi ni hatari kwa timu yake.

Wabongo wapenda sifa na umaarufu watakuja na vicochi vyenye madhara wakitegemea kutrend mitandaoni na umaarufu huo.

Hajafikiria mara 2, kaanza kua msemaji uchwara sasa.
 
Ulisikia wapi kuwa vitochi vinaleta madhara kwenye mpira? Vitochi vilikuwepo toka enzi hizoo za akina kaseja... na huwa vinatumiwa na mashabiki wa timu zenye malengo kama al hally, zamalek, simba..au timu za taifa zenye malengo kama senegal, misri... we unafikiri kwa mfano utopolo vs polis tz zikicheza unaweza kuona vitochi? Acha semaji liendelee kufanya mambo yake...
 
Wapendwa nimemuona msemaji wa Simba huko YouTube akimtembelea na kumpongeza mzee aliyekuwa na kitochi uwanjani. Hii si sawa kwani anahamasisha vitendo vya utovu wa nidhamu unaoweza kuigharimu timu.

Kesho watu wakija na vitochi zaidi tena vyenye mwanga wenye madhara atafanyaje? Nilitegemea angekemea huo upuuzi lakini ndio kwanza ana uhamasisha.

Brother, wewe ni msemaji wa club kubwa, achana na vitu vya hovyo visivyo na tija.

NB: Niko tayari kwa povu.
Aya nenda ww kawe msemajeee🤣🤣🤣 maaaana nchiii kula mtu mchambuziiii na msemaje
 
....
IMG_20220405_145117.jpg
 
Wapendwa nimemuona msemaji wa Simba huko YouTube akimtembelea na kumpongeza mzee aliyekuwa na kitochi uwanjani. Hii si sawa kwani anahamasisha vitendo vya utovu wa nidhamu unaoweza kuigharimu timu.

Kesho watu wakija na vitochi zaidi tena vyenye mwanga wenye madhara atafanyaje? Nilitegemea angekemea huo upuuzi lakini ndio kwanza ana uhamasisha.

Brother, wewe ni msemaji wa club kubwa, achana na vitu vya hovyo visivyo na tija.

NB: Niko tayari kwa povu.

Screenshot_20220404-185910.png
 
Hizi laser hazina madhara yeyote wachezaji wanamulikwa hata macho hawafumbi
 
Back
Top Bottom