Msemaji wa Singida Fountain Gate FC Hussein Massanza umewasikia lakini Wana Mkoa wa Singida (Watani Zangu) na Tamko lao hili takatifu na tukuka?

Msemaji wa Singida Fountain Gate FC Hussein Massanza umewasikia lakini Wana Mkoa wa Singida (Watani Zangu) na Tamko lao hili takatifu na tukuka?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
"Tumeshachoka sasa na hii tabia ya Uongozi wa Singida Fountain Gate FC ya kila mara kubadili Jina la Timu, kuhamisha Timu kwenda Mikoa mingine na kufanya Biashara kimya kimya ambazo hazileti Tija kwa Timu yetu.

Sisi wakazi wa Singida tunaomba hii Timu ibadilishwe Jina na watumie Majina ya huko wanakoenda badala ya kutumia Jina la Mkoa wetu wa Singida halafu Wanafungwa hovyo hovyo tu na kuishushia Hadhi Singida yetu na wana Singida wote ambao wanajulikana kwa umakini wao mkubwa" amesema leo Shabiki wa Singida Fountain Gate FC kupitia Kipindi cha Michezo cha E-SPORT cha EFM Radio.

Cc: Hussein Massanza
 
"Tumeshachoka sasa na hii tabia ya Uongozi wa Singida Fountain Gate FC ya kila mara kubadili Jina la Timu, kuhamisha Timu kwenda Mikoa mingine na kufanya Biashara kimya kimya ambazo hazileti Tija kwa Timu yetu.
Anachanigia nini kwenye timu?
 
Back
Top Bottom