Msemaji wa Yanga H. Bumbuli amporomoshea matusi Msemaji wa Simba H.Manara!

Msemaji wa Yanga H. Bumbuli amporomoshea matusi Msemaji wa Simba H.Manara!

Freyzem

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2013
Posts
10,120
Reaction score
24,667
Kuna clip inasikika ambayo, msemaji wa Yanga ndugu H.Bumbuli anamporomoshea matusi makubwa na kumdhalilisha msemaji wa Simba ndugu Haji Manara!

Amesikika akimkebehi kwa kuwa alibino, na kutoa maneno ambayo kiukweli hayafai katika jamii!

Huyu Bumbuli alifanywa kitu na Manara kiasi cha kumporomoshea matusi mazito hivyo Manara..!?

Kama ni masuala ya mpira tu, hata kama ni mambo mengine, amekosea sana!

Mpira siyo uhasama, kuwa watani wa jadi siyo kutukanana na kudhalishana!

...Bumbuli, anafaa achukuliwe hatua stahiki ili iwe fundisho!

Hata na hivyo Haji Manara amekuwa mstaarabu na kusema kuwa anamsamehe kwa aliyoyafanya! Hiki alichofanya Haji ni ustaarabu lakini, hili linaweza kujitokeza tena kwa mwingine na ikawa ni mazoea kudhalilishana ama kutukanana kisa mambo ya mpira, ambao kwa kweli ni burudani kwa walio wengi!

Hiyo clip najaribu kuipandisha inagima hapa!

Naamini wapo wenye hiyo clip, ila pitia hapa utaweza kuiona!

 
Hata wewe ni mpumbavu mnateteana wapumbavu
Huyo Haji wenu akitukana ni halali lakini akijibiwa lelele wapumbavu

Ni hasira za nini mkuu hizo unataka kuzimalizia hapa?
...tuliza jazba kijana usipanic!

Haya sawa mimi mpumbavu, hasira zimeisha dogo?

Now twende sasa, hebu eleza hapa ni lini na wapi Haji alishawahi kutukana matusi makubwa na kudhalilisha utu wa mwingine kama alivyofanya Bumbuli?

Wote tunafahamu Haji ana maneno makali ya ule utani wa jadi kama ilivyokuwa Jerry Muro sasa kama hayo maneno yanawaidhi baadhi ya watu hapaswi kutukanwa tena kudhalilishwa kuwa yeye ni albino n.k! Anapaswa ajibiwe either kwa hoja au mipasho hiyo hiyo ambayo haigusi utu ama asili yake!

...Ikitokea Haji katukana siwezi kumtetea, sasa kama wewe unasema anatukana leta ushahidi hapa!
 
Ila msomi wa madrasa akiporomosha matusi ni sawa, wengine wachukuliwe hatua

Weka hayo matusi hapa kijana!
...halafu utambue kuwa ukitukanwa nawewe unajusification ya kurudisha matusi!!
Weka clip/ushahidi unaoonyesha Haji akimtusi mtu kuwa ni ms*** ama tusi lolote, au akimdhalilsha mtu utu wake n.k!
 
Aombe radhi Manara hakupenda awe albino

Na huo ndio ustaarabu, ubaguzi wa aina yoyote haukubaliki!
...si ajabu hao wanaonyanyapaa albino wakazaa watoto albino pia!!
Kwani wazazi wa Manara ni albino!?
 
Haji ni mchokozi,ana maneno ya kuudhi sana. Huwa anatukana sana,ila anaachwa tu. Hapo ni haji alirekodi sehemu ya mazungumzo binafsi, hakuna sehemu ya mwanzo ya mazungumzo yao.
 
ukijiheshimu utaheshimiwa tu, kiukweli huyo mtu, kama anachukia maneno kama hayo, inabidi ajitathmini sana ye mwenyewe na aina yake ya uropokaji, kejeli n.k. kwa mtazamo wangu, huyo jamaa hiki si kipindi sahihi kwake kuwa msemaji wa klabu kubwa na yenye heshima kama simba! roporopo mno na vijimaneno maneno vingi visivyo na maana ....... asitafute huruma kwa kupitia ulemavu wake!
 
Hapa usimba na uyanga umeshaingia. Busara ni wamalizane wao wenyewe kisheria ama kwa kusameheana, haina maana wanajukwaa pia kuanza kutunishiana misuli kwa matusi, si culture ya JF
 
Sasa kwani Haji siyo zeruzeru? Mbona unakuwa mbaguzi hivyo?

...amembagua nani?

Haji ni albino kweli, lakini kumkashifu yeye kwa kuutaja ualbino wake hiyo si sawa!

Kuwa albino ni ulemavu, sasa inapotokea mtu unamkashifu kisa ni mlemavu na wewe upo sawa hiyo si haki!
Natumaini unaelewa hili vyema...
 
Watu wanajadili kiushabiki wamesahau kocha wa timu ya taifa uingereza alijiuzulu kutokana na kauli yake kuwa walemavu ni watu waliolaaniwa na Mungu anapozungumzia Haji kama Albino anahusisha kundi kubwa ambalo halihusiki kwenye malumbano yao
 
Back
Top Bottom