Freyzem
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 10,120
- 24,667
- Thread starter
- #21
ukijiheshimu utaheshimiwa tu, kiukweli huyo mtu, kama anachukia maneno kama hayo, inabidi ajitathmini sana ye mwenyewe na aina yake ya uropokaji, kejeli n.k. kwa mtazamo wangu, huyo jamaa hiki si kipindi sahihi kwake kuwa msemaji wa klabu kubwa na yenye heshima kama simba! roporopo mno na vijimaneno maneno vingi visivyo na maana.......asitafute huruma kwa kupitia ulemavu wake!
Haji sidhani kama anatafuta huruma!
Kama Bumbuli asingetaja ulemavu wake naamini wangemalizana pengine kimya kimya au asingeumia sana!
Bumbuli kuutaja kumdhalilisha kwa kuutaja ualbino wake haimuumizi haji peke yake, hata albino wengine pia wanaumia!
Wapo albino ambao pia ni mashabiki wa yanga, watajisikiaje kwa hayo maneno kutoka? Yupo mchambuzi mmoja wa soka ambaye pia ni mtangazaji,anaitwa Zungu sasa haya maneno aliyotoa Bumbuli zungu atayachukuliaje pamoja na albino wengine!?
...leo ikiwa pia ni siku ya albinism, unyanyapaa au udhalilishaji kwao haufai!