Msemaji wa Yanga Haji Manara aufyata, amuomba radhi Rais wa TFF Wallace Karia

Msemaji wa Yanga Haji Manara aufyata, amuomba radhi Rais wa TFF Wallace Karia

Binafsi kama shabiki wa Yanga SC ninashikuru kuwa ameomba msamaha ili aendelee kuwapo kwa lengo la KUKINUKISHA ZAIDI.
Wapewa dozi watakua wamenuna hili jambo la kuomba msamaha japo watajifanya wanamdhihaki haji lakini mioyoni wameumia
 
Wanaomchukia kama nani?

Halafu msamaha wenyewe umeombwa kwa shinikizo, inaonekana uongozi wa Yanga ndio umemshauri aje aombe radhi

So busara yake hapo iko wapi?

Huyu mtu bado anasimamia msimamo wake, huo msamaha ni takwa la club kulinda maslahi yake lakini mimi na wewe wote tunajua Manara asingeweza kuthubutu kwa willing yake kuomba radhi
Na hili litawapa shida sana Yanga, kwasababu hawawezi kujitenga na Kauli zake..!
 
Msemaji wa Yanga Haji Manara ameufya kwa kuamua kujishusha baada ya kumuomba radhi Rais wa TFF Wallace Karia kuhusu jambo ambalo lilitokea Jijini Arusha wakati wa fainali la Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup ASFC, baina ya Yanga SC na Coastal Union.

"Jana mimi na rafiki yangu Heris Said alinisindikiza kwenda kumuona Rais wa Shirikisho la Soka Nchini Tanzania Wallace Karia, na tuliongea kwa furaha sana na kuzungumza mambo ya msingi zaidi nyumbani kwake.

"Kiukweli jambo la Arusha tukio zima halikua na matusi, hilo nataka iwe Very Clear, ambalo watu wengi wananishtumu nalo na waling'ang'ania hapo hapo.

"Ndo maana nilisema pale Airport, kuwa atakayepata tukio lile likiwa na matusi nitajiuzulu kwa kuwa nitakuwa kinyume na hata maadili ya kitanzania na wala si football peke yake.

"Naomba msamaha kwa namna yoyote ile nilikosea kujibizana na Rais Wallace Karia naomba radhi, haimaanishi mini nisichukuliwe hatua.

Kama itaonekana nastahili kuchukuliwa hatua nipo tayari kupokea adhabu hiyo, lakini lazima niombe msamaha bila kujali kamati itaamua nini.

Kingine sina matatizo na Karia, ni Mzee wangu na namheshimu, na nimekuwa mstari wa mbele mara kadhaa kutetea hoja zake.

Naomba radhi, mimi ni mwanadamu na binadamu yoyote yule hukosea, ila kwa kuwa Rais amenizidi kwa vitu vingi sana, sina budi kuheshimu na kuomba radhi kubwa kwake, amenizidi umri na mambo mengi ambayo itakuwa si uungwana kuliacha jambo hili."

Amezungumza Haji Manara kwenye mkutano wake na waandishi wa vyombo vya habari, kufuatia kadhia yake na Rais wa TFF Wallace Karia.
Hakuna cha msamaha wala nini.

Kamati ya nidhamu impe hukumu kali ili ajifunze kuheshimu watu

Kutukana wengine manara hakuanza leo.

Ni kitu amekuwa akikifanya karibu kila mara na ushahidi upo. Amezoea.

Miaka kumi ya yeye kutojihusisha na mpira itakuwa adhabu sahihi kwake.
 
Wangelitaka hilo Safari yenu ya kutwaa ubingwa ingewashinda mapema.

Ingewezekana. Nakubali.

Wangeanzisha kanuni mpya ambayo itaruhusu timu yeyote kuwa na zaidi ya wachezaji 13 ndani ya uwanja.

Hapo wangetuweza.

Ila tofauti na hapo, hakuna chochote wangeweza kufanikiwa
 
Ingewezekana. Nakubali.

Wangeanzisha kanuni mpya ambayo itaruhusu timu yeyote kuwa na zaidi ya wachezaji 13 ndani ya uwanja.

Hapo wangetuweza.

Ila tofauti na hapo, hakuna chochote wangeweza kufanikiwa
Umesahau mlivyojiliza miaka 4 eti mnaonewa na Simba inabebwa.
 
Viongozi wa Yanga SC wana akili sana.

Wameshaufahamu uongozi wa Msomali Karie unachotaka. Si kingine bali ninkuidhoofisha Yanga SC wakidhani wanaikomoa.

Wakamshauri akaombe msamaha wakijua wazi msamaha utaondoa adhani ya kufungiwa na kubakisha adhabu ya faini.

Ambayo hata iyo faini inaweza kusamehewa pia.
Msamaha hauondoi sheria na kanuni kutofanya kazi..! Vipo kwa ajili ya kufanya kazi
 
Jambo limeisha hilo......hata hiyo kamati ina njaa vilevile,Manara atapigwa faini ya milioni 10 na zitalipwa na GSM kwasababu ndio anaowafanyia kazi

Kamati ya nidhamu watagawana mpunga wao na Manara ataendelea kuwakera watu kama kawaida yake
 
Msemaji wa Yanga Haji Manara ameufya kwa kuamua kujishusha baada ya kumuomba radhi Rais wa TFF Wallace Karia kuhusu jambo ambalo lilitokea Jijini Arusha wakati wa fainali la Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup ASFC, baina ya Yanga SC na Coastal Union.

"Jana mimi na rafiki yangu Heris Said alinisindikiza kwenda kumuona Rais wa Shirikisho la Soka Nchini Tanzania Wallace Karia, na tuliongea kwa furaha sana na kuzungumza mambo ya msingi zaidi nyumbani kwake.

"Kiukweli jambo la Arusha tukio zima halikua na matusi, hilo nataka iwe Very Clear, ambalo watu wengi wananishtumu nalo na waling'ang'ania hapo hapo.

"Ndo maana nilisema pale Airport, kuwa atakayepata tukio lile likiwa na matusi nitajiuzulu kwa kuwa nitakuwa kinyume na hata maadili ya kitanzania na wala si football peke yake.

"Kwa namna yoyote ile naomba msamaha, nilikosea kujibizana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Tanzania Wallace Karia, naomba radhi, na haimaanishi mimi nisichukuliwe hatua.

Kama itaonekana nastahili kuchukuliwa hatua nipo tayari kupokea adhabu hiyo, lakini lazima niombe msamaha bila kujali kamati itaamua nini.

Kingine sina matatizo na Karia, ni Mzee wangu na namheshimu, na nimekuwa mstari wa mbele mara kadhaa kutetea hoja zake.

Naomba radhi, mimi ni mwanadamu na binadamu yoyote yule hukosea, ila kwa kuwa Rais amenizidi kwa vitu vingi sana, sina budi kuheshimu na kuomba radhi kubwa kwake, amenizidi umri na mambo mengi ambayo itakuwa si uungwana kuliacha jambo hili."

Amezungumza Haji Manara kwenye mkutano wake na waandishi wa vyombo vya habari, kufuatia kadhia yake na Rais wa TFF Wallace Karia.
Si alisema anataka kugombanishwa na viongozi wa TFF, ?
 
Umesahau mlivyojiliza miaka 4 eti mnaonewa na Simba inabebwa.

Asiye na akili ndiye aliyekuwa akilia.

Je mimi ni miongoni mwao? Bila shaka hapana. Hatukuwa vyema ndio maana hatukutwaa tuzo katika kipimdi hiko.
 
Na hili litawapa shida sana Yanga, kwasababu hawawezi kujitenga na Kauli zake..!

Ndio kwanza kamaliza mwaka akiwa Jangwani.

Kama ambavyo mliweza kumvumilia nyinyi kwa miaka 5, ndivyo Wananchi watakavyo weza kumvumilia kwa miaka 5 ijayo.
 
GSM wameishika TFF.ipo mfukoni mwao.
Ni baada ya mkutano wa leo.

Ivyo akuna cha kamati wala nn.
Screenshot_20220705-201820_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom