Msemaji wa zamani wa Simba Asha Muhaji amefariki dunia

Msemaji wa zamani wa Simba Asha Muhaji amefariki dunia

AKILI TATU

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2016
Posts
2,659
Reaction score
2,827
Aliyekuwa msemaji wa Simba miaka ya 2010-12 Asha Muhaji ametangulia mbele ya haki mchana huu.

mungu amrehemu

images (1).jpeg

Asha Muhaji enzi za uhai wake
======


Dar es Salaam. Aliyekuwa afisa habari wa Simba SC na mwandishi wa habari za michezo, Asha Muhaji amefariki dunia mchana wa leo, Jumatano.

Asha (50) amekutwa na mauti wakati anaendelea na matibabu hospitali ya Hindu Mandali iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mdogo wa marehemu, Habibu Kaumo alithibitisha kifo cha dada yake kuwa kilitokana na kusumbulia na TB ya ngozi iliyogundulika baada ya kufanyiwa vipimo juzi Jumanne.

Alisema kuwa marehemu mara kadhaa alikuwa akiumwa, lakini tatizo hilo halikugundulika hadi alipopelekwa katika hospitali hiyo ambako alilazwa tangu Alhamisi ya wiki iliyopita.

"Alikuwa anaumwa na mwili wake ulikuwa ukidhoofika kadri siku zinavyokwenda bila kujua tatizo kuwa ni TB ya ngozi ambayo awali haikujulikana kama anayo," alisema na kuongeza

"Baada ya vipimo ndipo amegundulika kuwa ana tatizo hilo lakini akiwa katika hali mbaya sana ya kupumulia mashine, madaktari wamejitahidi kadri ya uwezo wake, lakini Mungu ameamua kumpumzisha mchana wa leo." alisema

Habibu alisema msiba upo nyumbani kwa wazazi wake Mabatini, Kijitonyama ambapo mazishi yatafanyika leo Alhamisi kwenye makaburi Mwinyimkuu yaliyopo Magomeni, Dar es Salaam.

"Tumeutoa mwili hospitalini na kwenda kuuhifadhi msikiti wa Mahmuru uliopo Upanga ambapo kesho leo atafanyiwa ibada kabla ya kuelekea makaburi kumpumzisha, marehemu hajaacha mtoto" alisema

Asha enzi za uhai wake aliwahi kufanyakazi kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Uhuru na New Habari akiwa mhariri wa michezo gazeti la Rai.

Chanzo: Mwananchi
 
RIP afisa wa habari wa Simba SC, Asha Muhaji. Poleni wanafamilia, chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA, marafiki na wana Msimbazi. Anaonekana alikuwa mwana habari nguli kwa jinsi alivyoongea kwa weledi mkubwa.

 
R.I.P

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹ [emoji377]
 
Apumzike kwa Amani apate raha na Starehe ya Milele huko Mbinguni
 
Back
Top Bottom