Msemo gani wa kiswahili unakukera?

Msemo gani wa kiswahili unakukera?

"Shoga yangu "
Yaani nikisikia hilo neno nakereka, hata kama waschana /wanawake wanaitana hivo.
Kwa nini wasiitane "rafiki"
Kwan lazima kusema ushoga
 
"Muungwana akivuliwa nguo huchutama" huu msemo bwana,sasa mambo ya kuvuliwa nguo afu unachutama,yakheee hii sio sawa[emoji85][emoji1787][emoji1787]
 
"Jiongeze" - Sijui kwanini huwa wanaamini mpaka hapo nilipofika sikujiongeza

"Sio rahisi kama unavyodhani" - Unajuaje kwamba nadhani ni rahisi. Mbaya zaidi unajua hadi 'kiasi ninachodhani'
 
nikisikia PDF imetema halafu nikiwaza sikuweka barua ya kujitolea kwenye kuomba ajira
 
'Naniliu/ nanilii'. Hata sielewi limetokea wapi?
 
" Haipingwi" na "Sheria"sijui yana maana gani hauo maneno ya kihuni.
 
"Muungwana akivuliwa nguo huchutama" huu msemo bwana,sasa mambo ya kuvuliwa nguo afu unachutama,yakheee hii sio sawa[emoji85][emoji1787][emoji1787]
Sasa umeshawahi kuona wapi mtu akivuliwa nguo au kanga ikspeperushwa na upepo mtu akasimama wima? Lazima uchuchumae (kuchutama) ili kuficha zana za kazi zisionekane...
 
Back
Top Bottom