Msemo wa jadi wa kichina: “Mtu hapaswi kubadili ahadi yake au kuacha harakati zake hata kama anakabiliwa na hatari”

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121

Mkutano wa mwaka wa Baraza la Asia la Boao ulifanyika kuanzia Jumatano hadi Ijumaa wiki hii huko Boao, mkoani Hainan, kusini mwa China. Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “COVID-19 na dunia: kuhimiza kwa pamoja maendeleo ya dunia na kujenga mustakbali wa pamoja”.

Kuna msemo mmoja wa Kichina unasema “Mtu hapaswi kubadili ahadi yake au kuacha harakati zake hata kama anakabiliwa na hatari” Msemo huu unaelezea juu ya namna dunia inavyoweza kukabiliana na majanga mbalimbali na hatimaye kuyashinda, mathalan namna ya kupambana na janga la COVID-19 na namna ya kujenga ulimwengu baada ya janga hili.

Alipohudhuria mkutano wa Baraza la Uchumi la Dunia kwa njia ya video mwaka huu, rais Xi Jinping wa China alinukuu msemo huo maarufu akisema "Siku zote ulimwengu unaendelea kupitia kwenye harakati zinazokinzana; bila kukinzana, kisingekuwepo kitu."Historia ya binadamu ni historia ya kufikia ukuaji kwa kukumbana na majaribio mbalimbali, na kukua kwa kushinda majanga mbalimbali. Tunahitaji kusonga mbele kwa kufuata mantiki ya maendeleo ya kihistoria, na kukua kwa kupanda wimbi la maendeleo ya nyakati zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…