Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Mtangazaji maarufu wa soka nchini Tanzania, Baraka Mpenja, amejikuta katikati ya kimbunga cha malalamiko kutoka kwa mashabiki wa soka nchini baada ya kutuhumiwa kuonyesha upendeleo wa wazi na kusifu uwekezaji wa Gharib Said Mohamed (GSM) ndani ya Yanga SC badala ya kuzingatia utangazaji, mbinu na ufundi wa mchezo uwanjani.
Mashabiki wameeleza kutoridhishwa kwao na namna Mpenja anavyotangaza mechi za Yanga SC, wakidai kuwa amekuwa akitumia muda mwingi kusifu uwekezaji wa GSM na klabu hiyo badala ya kueleza mbinu na mfumo wa mchezo.
Akijibu mashambulizi hayo kwenye mitandao ya kijamii, Mpenja alijibu kwa kejeli akisema: "Mimi siyo kocha, sijui mbinu na ufundi wa wachezaji... njoo uwe chawa na wewe baaasi," kauli iliyozidisha majibizano na mashabiki.
Baadhi ya mashabiki wa Simba walifikia hatua ya kumwambia hawataki atangaze michezo ya Simba SC, ambapo Mpenja alijibu kwa mkato:
"Mimi nawataka sasa?" huku akiwataka wanaomkosoa "kurudi shule" kujifunza maana ya utangazaji na utambulisho (identity).