Mshabiki wa soka nchini wamvaa mtangazaji Baraka Mpenja

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Mtangazaji maarufu wa soka nchini Tanzania, Baraka Mpenja, amejikuta katikati ya kimbunga cha malalamiko kutoka kwa mashabiki wa soka nchini baada ya kutuhumiwa kuonyesha upendeleo wa wazi na kusifu uwekezaji wa Gharib Said Mohamed (GSM) ndani ya Yanga SC badala ya kuzingatia utangazaji, mbinu na ufundi wa mchezo uwanjani.

Mashabiki wameeleza kutoridhishwa kwao na namna Mpenja anavyotangaza mechi za Yanga SC, wakidai kuwa amekuwa akitumia muda mwingi kusifu uwekezaji wa GSM na klabu hiyo badala ya kueleza mbinu na mfumo wa mchezo.

Akijibu mashambulizi hayo kwenye mitandao ya kijamii, Mpenja alijibu kwa kejeli akisema: "Mimi siyo kocha, sijui mbinu na ufundi wa wachezaji... njoo uwe chawa na wewe baaasi," kauli iliyozidisha majibizano na mashabiki.

Baadhi ya mashabiki wa Simba walifikia hatua ya kumwambia hawataki atangaze michezo ya Simba SC, ambapo Mpenja alijibu kwa mkato:
"Mimi nawataka sasa?" huku akiwataka wanaomkosoa "kurudi shule" kujifunza maana ya utangazaji na utambulisho (identity).

Mwenyezi Mungu amjalie Hekima na busara, Amwondolee kiburi.....

Vinginevyo, hana maisha marefu kwenye utazangaji wa boli...
 
Na yeye ana mwiiko nyuma. Anyway back ground yake ichunguzwee.
 
Nimelipenda jibu la Mpenja kwa mashabiki wa Simba, kwamba kenyewe kanawataka sana! Mashabiki wa Simba nao watumie akili aisee!
 
Kwanza amejitahidi kuwajibu Kwa sitaha maana hamna akili wewe na wapuuzi wenzio.
 
Daah Bongo watu mmedumaa sana yaani mna makasiriko kama wanawake wenye Mimba mtu kumtaja GSM au Mo ninyi shida nini kama unaona anafaidi na wewe tafuta chaka lako litangaze mnagombana kwa vitu vya kijinga jinga tu..
 
Unawaongelea mashabiki wa Tz ambao timu inapoteza mechi wao wanaamini ni kwakua msemaji wa timu kaondoka
 
mambo yenu daslamu hayo sie hatuyajui
 
Daah Bongo watu mmedumaa sana yaani mna makasiriko kama wanawake wenye Mimba mtu kumtaja GSM au Mo ninyi shida nini kama unaona anafaidi na wewe tafuta chaka lako litangaze mnagombana kwa vitu vya kijinga jinga tu..
Mkuu sema Simba usiseme Wabongo!
 
Unawaongelea mashabiki wa Tz ambao timu inapoteza mechi wao wanaamini ni kwakua msemaji wa timu kaondoka
Shida ni nini mkuu mbona watu bongo zao zimelala sana kama walimwagiwa maji ya Udumavu..
 
Hao mashabiki watakua ndiyo wale walioitwa mbumbumbu na mwenyekiti mstaafu Ismail Aden Rage.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…