Mshahara ulitoka juzi, umebakisha sh. Ngapi wewe adi saa hii!!

Kuna jamaa mmoja ana mikopo hatari kwenye taasisi za fedha, yeye kwa sasa mshahara wake ni Tzs 15,000/- anazobaki nazo. Sijui atakuwa na buku ngapi mpaka leo?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] huyo jamaa sio wewe kweli?[emoji3] [emoji3] [emoji3] sema ukweli bwana kwann uzunguke mbuyu
 
Hv kwann kwa sisi tulio wengi mshahara huwa haukutani na wa mwezi unaofuata...yan tatizo nini wakubwa?
Mpangilio mbaya wa bajeti, watumishi wengi mshahara ukitoka huweka shida chini na kutupa mikono juu,yaan wana banjuka tu kwenye misosi,kwenye vinywaji na kila aina ya starehe baada ya wiki tu hayo yanabaki story, binafsi nikishapata mshahara Mara baada ya kutumia wazazi fungi flani kwa ajili ya kuwa support hutuliza kichwa chini kwa kula maharage na mamboga yasiyoeleweka wiki nzima ya kwanza ili kufanya mgawanyo wangu kwa kuzingatia vipaumbele next weeks zinazofuata ndio huanza kula kwa kujitanua based on targeted budget
 
mshahara upi wa December au? maana November nilisha sahau kama nilipokea
 
Vipi unafamilia au ni bachela?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] huyo jamaa sio wewe kweli?[emoji3] [emoji3] [emoji3] sema ukweli bwana kwann uzunguke mbuyu
😀Hapana mimi sio mtumishi wa serikali. Jamaa yangu niliyesoma naye university ndio aliyenipa story hii ya mwalimu mwenzie.
 
Hv kwann kwa sisi tulio wengi mshahara huwa haukutani na wa mwezi unaofuata...yan tatizo nini wakubwa?
Coz tunaishi kwakukopa ikifika mwisho wamwezi unakimbiza pesa kwa mangi na kilabuni Sasa hapo mishahara itakutana vip kwamfano[emoji12] [emoji12]
 
Jamaa mmoja mwalimu, anadaiwa tayari tshs. 295,000 na kapokea mshahara juzi..

Alikuwa na madeni sana, tatizo ana wake wawili, hili ndio tatizo lake.. tulimshauri asioe mke wa pili hakusikia..
Uzuri wake, hawezi kuumwa na kichwa wote wawili kwa mpigo.
 
Ni kanuni ya uchumi wa kifedha huo, kwanza pesa haiwezi kujililinda yenyewe, pili walinzi wake hulipwa kwa kuitafuna hiyo fedha yenyewe, mwisho fedha "haiwezi, haijawahi kuweza, na haitakujawahi kuweza kymtosheleza yeyote.
 
Aliye mtumwa wa uchumi wa kifedha ni mtumwa wa kudumu milele.
 
Hakuna pesa inayotosha..
Hili nalo neno! Kuna jamaa yangu anapokea cash 3M+ lakini mara nyingi inapokaribia mwisho wa mwezi huwa ameishiwa kabisa. Ila yeye amewekeza kwenye bia labda ndio sababu!
 
Kabla haujaingia, ulishafekwa na HESLB, TRA, PPF na NHIF. Kinachobaki na bank charges
 
2300.55

msema kweli ni mpenzi wa mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…