Mshahara umeingia lakini umeshaisha tayari

Mshahara umeingia lakini umeshaisha tayari

Let's dance the same song, stress zinafuata Kisha hasira na kukata tamaa, shetani anakucheki kwa mbaali huku anacheka tu🤣🤣

Mshahara ni kama tembo ukiwa haujatoka, ila ukitoka tu unaona kama kasungura Fulani hivi.🤣
 
Kwa huu mshahara wa watumishi wengi wa kima cha chini na wale wa kima cha kati; maana yake:-
1. Hutakiwi kumsomesha mtoto/watoto wako shule binafsi.
2. Hutakiwi kukopa benki na kufanyia kitu chochote mfano kununua gari, kujenga nyumba, nk.
3. Hutakiwi kumsaidia mtu yeyote yule fedha itokanayo na hio mshahara! Yaani wakiwemo wazazi na ndugu zako.
4. Hutakiwi kufanya maendeleo yoyote yale! Yaani hela yako inatakiwa iwe ni kwa ajili ya kula, kuvaa kwa mbali, nk.

Ila cha kushangaza kwa wale wafanyakazi wachache wa kima cha juu; wao kila siku ni sherehe tu. Maana wana hela mpaka wengine wanaamua kuanzisha miradi/biashara za kuzitakatisha hizo fedha.
 
Back
Top Bottom