Mshahara umeingia lakini umeshaisha tayari

Mshahara umeingia lakini umeshaisha tayari

Tuungane pamoja tuanzishe chama chetu wale mshahara unaoishia hewani ata masaa 24 hayafiki
Pia kwa wale ambao mishahara yao inakwisha hata kabla hawajaipokea. Hapa namaanisha wale wenye mikopo ya kausha damu ambao Kadi zao za Benki zimechukuliwa na hao wanaowadai. Pindi wapatapo taarifa za kuingiziwa mshahara wanakwenda kuzikomba zote bila huruma.
 
Kwa huu mshahara wa watumishi wengi wa kima cha chini na wale wa kima cha kati; maana yake:-
1. Hutakiwi kumsomesha mtoto/watoto wako shule binafsi.
2. Hutakiwi kukopa benki na kufanyia kitu chochote mfano kununua gari, kujenga nyumba, nk.
3. Hutakiwi kumsaidia mtu yeyote yule fedha itokanayo na hio mshahara! Yaani wakiwemo wazazi na ndugu zako.
4. Hutakiwi kufanya maendeleo yoyote yale! Yaani hela yako inatakiwa iwe ni kwa ajili ya kula, kuvaa kwa mbali, nk.

Ila cha kushangaza kwa wale wafanyakazi wachache wa kima cha juu; wao kila siku ni sherehe tu. Maana wana hela mpaka wengine wanaamua kuanzisha miradi/biashara za kuzitakatisha hizo fedha.
uko sahihi mkuu, yani ikipungua 50 tu, ushavuruga kila kitu.
 
Dunia ukilemaa upati kitu kabisa hupati kitu kabisaa (unamfahamu uyo msanii)???
 
Back
Top Bottom