Kwa huu mshahara wa watumishi wengi wa kima cha chini na wale wa kima cha kati; maana yake:-
1. Hutakiwi kumsomesha mtoto/watoto wako shule binafsi.
2. Hutakiwi kukopa benki na kufanyia kitu chochote mfano kununua gari, kujenga nyumba, nk.
3. Hutakiwi kumsaidia mtu yeyote yule fedha itokanayo na hio mshahara! Yaani wakiwemo wazazi na ndugu zako.
4. Hutakiwi kufanya maendeleo yoyote yale! Yaani hela yako inatakiwa iwe ni kwa ajili ya kula, kuvaa kwa mbali, nk.
Ila cha kushangaza kwa wale wafanyakazi wachache wa kima cha juu; wao kila siku ni sherehe tu. Maana wana hela mpaka wengine wanaamua kuanzisha miradi/biashara za kuzitakatisha hizo fedha.