Mshahara wa Daktari ni kiasi gani?

Mshahara wa Daktari ni kiasi gani?

paqwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2019
Posts
2,106
Reaction score
2,831
Katika kada inayoongoza kwa kulaumiwa na kuonewa ni afya. Sasa viongozi wa kada hiyo ni madaktari maana ndio moyo. Nataka kujua, wanalipwa kiasi gani mpaka wanaonewa kiasi hicho?

Tulinganishe na watumishi mfano wa WCF, NSSF, PSSSF, TRA, TISS bila roho mbaya wala husda, nani anafanya kazi ambayo atq bibi yako, wewe au ndugu yako popote alipo ni muhimu? Ni kweli mfanyakazi wa hapo DAWASA., anarisk kuliko daktari? Nipo Marekani, mimi ni epidemiologist japo sikufanya medicine, dhana ya udaktari ni wito haipo, wanapesa. Wanaheshimika sana.

Tanzania, wanatumia dhana ya wito kuwagandamiza ili wanapotaka kukaa sawa waonekane wana tamaa, hivi mtu aliepo pale TPA, anakula kiyoyozi, anatupia mafile, halaumiwi kwa lolote, ana mkopo wenye riba wanayojiwekea wenyewe, hajawahi kuamshwa usiku wala kurukiwa na damu ya mtu mwenye ebola au ukimwi ni wa kulipwa zaidi ya daktari? Dharau.

Tuna demand makubwa sana kutoka kwa hawa majamaa lakini kiukweli tunawaonea. Hii ni shida. Ila na wao vyombo vyao vinawasaliti kwakuwa viongozi wao wanalamba asali lakini sio sawa. Nilitamani kuwa daktari ila nashukuru niliona mbali. Yani kutoka kwao ni balaa hapo Tanzania. Inatia huruma, watu mpaka familia zinawasahau.

Ni janga Tanzania. Siasa inaleta dharau. Nikiuliza babu tale, individually amefanya nini leo au jana chenye impact kuliko mtu alietoa busha au kufanya operation, kweli? Kuna pahala hapako sawa. Na mkiendekeza siasa mtajua hamjui.
 
Inategemea na mwajiri ni nanj .

Maana kuna wengine wanafanya chini ya Tamisemi.

Wengine wizara ya afya.

Wengine kwenye taasisi za kiserikali kila mmoja na mshahara wake japo kada ni moja.

Na unapoongelea Daktari.

Kuna MD
Kuna specialist.
Kuna Daktari bigwa .
Kuna Daktari mwandamizi.
 
Inategemea na mwajiri ni nanj .

Maana kuna wengine wanafanya chini ya Tamisemi.

Wengine wizara ya afya.

Wengine kwenye taasisi za kiserikali kila mmoja na mshahara wake japo kada ni moja.

Na unapoongelea Daktari.

Kuna MD
Kuna specialist.
Kuna Daktari bigwa .
Kuna Daktari mwandamizi.
Usipotoshe watu stick to one language.
Kuna
Daktari (GP)
Daktari bingwa (specialist)
Daktari mbobezi (consultant)
 
Inategemea na mwajiri ni nanj .

Maana kuna wengine wanafanya chini ya Tamisemi.

Wengine wizara ya afya.

Wengine kwenye taasisi za kiserikali kila mmoja na mshahara wake japo kada ni moja.

Na unapoongelea Daktari.

Kuna MD
Kuna specialist.
Kuna Daktari bigwa .
Kuna Daktari mwandamizi.
Naomba kujua tofauti ya ulivyoandika hapa kuwa kuna

Specialist
Daktari Bingwa

Kumbe hawa ni Watu Wawili tofauti?
 
Inategemea na mwajiri ni nanj .

Maana kuna wengine wanafanya chini ya Tamisemi.

Wengine wizara ya afya.

Wengine kwenye taasisi za kiserikali kila mmoja na mshahara wake japo kada ni moja.

Na unapoongelea Daktari.

Kuna MD
Kuna specialist.
Kuna Daktari bigwa .
Kuna Daktari mwandamizi.
Specialist ndio bingwa.
 
Sasa jamani unafanya kazi kwenye hospital inatibu wagonjwa 50 kwa siku, kila mgonjwa analipia elfu 20. Unataka kwa mwezi ulipwe Millioni 3 kweli?. Hizo hela za kukulipa hiyo pesa serikali inazitoa wapi.

Mwenzako anafanya kazi EWURA kama inspector, kila kwenye lita moja ya mafuta EWURA inachukua percent yake. Kila lita moja. Kwanini wasiwalipe wafanyakazi wao pesa ndefu?
 
Back
Top Bottom