Mshahara wa Daktari ni kiasi gani?

Mshahara wa Daktari ni kiasi gani?

Daktari anayeanza kazi basic ni TSH 1.3mil , take home 900+K...!!! Sema kuna viposho posho Kwa walio chini ya wizara ya Afya.... Maisha ni magumu Sana bado Kwa hawa watu, huwa wanakimbilia kwenye mikopo ya magar kuficha aibu...nazungumzia MD sio CO au tabibu
 
Nina mtoto Ni policcm na binti takitari.
Iko hv huyo Dogo Police ana professional yoyote level ya Degree kuanzia? Kama ni Form 4 leaver tu unadanganywa bado pakubwa ukijumlisha Salary+Posho ya mwezi na hata ukijumlisha allowance ya pango na packages hawezi kumfikia Daktree wa Tamisemi tu huo ndio ukweli ila kama Dogo ni Degree holder regardless kuwa ni Constable hapo nakiri atamzidi!!
 
Katika kada inayoongoza kwa kulaumiwa na kuonewa ni afya. Sasa viongozi wa kada hiyo ni madaktari maana ndio moyo. Nataka kujua, wanalipwa kiasi gani mpaka wanaonewa kiasi hicho?

Tulinganishe na watumishi mfano wa WCF, NSSF, PSSSF, TRA, TISS bila roho mbaya wala husda, nani anafanya kazi ambayo ara bibi yako, wewe au ndugu yako popote alipo ni muhimu? Ni kweli mfanyakazi wa hapo DAWASA., anarisk kuliko daktari? Nipo Marekani, mimi ni epidemiologist japo sikufanya medicine, dhana ya udaktari ni wito haipo, wanapesa. Wanaheshimika.

Tanzania, wanatumia dhana ya wito kuwagandamiza ili wanapotaka kukaa sawa waonekane wana tamaa, hivi mtu aliepo pale TPA, anakula kiyoyozi, anatupia mafile, halaumiwi kwa lolote, ana mkopo wenye riba wanayojiwekea wenyewe, hajawahi kuamshwa usiku wala kurukiwa na damu ya mtu mwenye ebola au ukimwi ni wa kulipwa zaidi ya daktari? Dharau.

Tuna demand makubwa sana kutoka kwa hawa majamaa lakini kiukweli tunawaonea. Hii ni shida. Ila na wao vyombo vyao vinawasaliti kwakuwa viongozi wao wanalamba asali lakini sio sawa. Nilitamani kuwa daktari ila nashukuru niliona mbali.

Ni janga Tanzania. Siasa inaleta dharau. Nikiuliza babu tale, individually amefanya nini leo au jana chenye impact kuliko mtu alietoa busha au kufanya operation, kweli? Kuna pahala hapako sawa. Na mkiendekeza siasa mtajua hamjui.
Ima uwaulize madaktari au uusomee udakatari. Je hii inakusaidia na kutusaidia nini?
 
We ndo huna akili na kama unazo za kushikiwa. Hujui kuwa hii haina faida hata kwa inzi!?
Watu tunataka wanaofanya kazi kweli, waheshimiwe au na we ni desk officer pahala unaenjoy semina na mshahara bila jasho? Watu wanajitoa, usiku umelala wanakesha, wanamwagikiwa damu za ukimwi, ebola ikija wanaanza kufa wao unataka tusihoji? Mbwa mwitu kweli
 
Back
Top Bottom