Mshahara wa dereva wa lori unaanzia kiasi gani hapa Tanzania?

Mshahara wa dereva wa lori unaanzia kiasi gani hapa Tanzania?

Ninja 1

Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
30
Reaction score
12
Habari zenu wana jamvi,

Kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nikitamani kujiunga na tasnia ya udereva particularly udereva wa malori (truck driver), nilikua naomba kujulishwa mshahara wa dereva wa lori apa Tanzania.

Asanteni
 
Wengi wao hawana mishahara, wanalipwa kwa route.

Ukipeleka Mzigo mfano nje ya nchi na ukarudi salama unapewa chako.

Unaweza Kupewa Laki 3 wakati wa kwenda, ukirudi unapewa laki 2.

Kama unaipenda fanya ila kiuhalali ni kazi ngumu na isiyo na kupumzika wala maslahi.

Madereva wengi wanategemea deal na kuibaiba.
 
Malipo ya uhakika ni ya mailej tu,kuna kampuni pia zinalipa mishahara ila baba uo mshahara unaweza uusikie tu.

ukipasua tairi unalipa kupitia uo mshahara wako,mzigo ukiibiwa ama kupotea wanakata mshahara,ukiibiwa mafuta sijui umeua betri au umeunguza brake drum unakatwa mshahara.

Ila ukipata kampuni nzuri yenye gari nzimana zinazotunzwa vizuri utakula maisha mpaka utasusa kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uta chapiwa mke

Nikiangaliaga zile foleni za malori pindi nnapoenda mkoa na gari ndogo na ule mwendo wao wanaotembea au zile foleni utakuta wamepangana kwenye halafu utakuta mtu anaenda nje ya nchi bado kila traffic hajakusimamisha kukupotezea muda zaidi aisee, najiulizaga huwa nachoka kabisa. Kufika sehemu inachukua masiku kibao barabarani.

Kuhusu kuchapiwa hata wao wenyewe wana makoloni yao kila kijiji wanapoweka kambi, wengine wanatembea kwenye magari yao kwa nyuma ya seat kunakuwa na sehemu ya kulala wanatembea na majiko kabisa popote wanaweka kambi wanapika na kula kisha wanalala, ila maisha bwana unaposema ya nini wenzako wanajiuliza wataipata lini.
 
Habari zenu wana jamvi,

Kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nikitamani kujiunga na tasnia ya udereva particularly udereva wa malori (truck driver), nilikua naomba kujulishwa mshahara wa dereva wa lori apa Tanzania.
Asanteni
Upo tayari uende kwa Sangoma...maana truck drivers wanapitia mengi na ni kazi hatarishi sana hasa safari za usiku barabarani.

Ila kazi ni kazi cha msingi mkono unaenda kinywani,vip ushawahi fikiria kuendesha magari ya ujenzi kufata vifusi afu ni usiku tu ndo hiyo kazi inafanyika hapa Dsm?
 
Back
Top Bottom