Mshahara wa dereva wa lori unaanzia kiasi gani hapa Tanzania?

~ makampuni mengi yanaonea madereva wao kudai mishahara kwa muda mrefu sana halafu mdogo....huwa ni lakini 2 na kuendelea,sifa ni kuendesha gari kubwa Benz,iveco,scania wengi wanalialia sana.
 
Habari zenu wana jamvi,

Kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nikitamani kujiunga na tasnia ya udereva particularly udereva wa malori (truck driver), nilikua naomba kujulishwa mshahara wa dereva wa lori apa Tanzania.

Asanteni
Niliwahi kua mhasibu wa kampuni moja yenye malori ya Mafuta.

Mshahara wa halali ilikua 250k - 400k

Posho (mileage) ukienda
Congo DRC 800k
Zambia 700k
Malawi, Burundi, Rwanda 600k

Ila posho hii nilikua nakata 100K, kwanza. Kuna siku tuliweka za kwenda na kurudi. Ukifanikiwa hizo siku basi 100k yako utaikuta. Ukichelewa hizo siku 100k imeenda.

Pia report ya kule mzigo unapoenda hutumwa huku head office. Kama mzigo umepokelewa pungufu nakukata posho ya safari ijayo.

Kwa mwezi madereva wangeweza kusafiri hata mara mbili.

Walikua wapiga dili njiani, anaeza uza mzigo kiasi kisha kule unakopokelewa akaongea na mpokeaji aeke hesabu vizuri wagawane.

Faida ingine ni kubeba mikaa ya kwake na ya kuuza akifika Dar. Pia Wanaoenda Zambia wanarudi na mchele Super bei ya Mbeya na vitu vingine kama hivyo.
 
Kwa mujibu wa kima cha chini cha mishahara ya mdereva ni laki mbili (200,000) kwa hiyo inabidi msharaha uanzie hapo na kuendelea ingawa makamluni mengi ya usafirishaji hawalipi mishahara unapewa tu ile posho ya safari ukienda na ukirud ambayo ni kidogo na pia inatofautiana kati ya kampuni moja na nyingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwastail hii madereva mshahara haujawahi kututosha kamwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mshahara wa dereva unaanza 100k-500k mkuu. posho ndo znawalisha maana mshahara c chochote!.. pia kwa hzo kazi ukifanya kampuni kubwa ndio kuna uafadhali maana hutasumbuliwa malipo yako.

mf. kampuni primefuels mshahara 150k ila safari ya kupeleka mzigo mfno geita ni 500k ukijibana mafuta katika uendeshaji wako pia ndo hvo unauza(reserve)

AZANIA- 250k mpka 400k wao pia posho ziko vzuri mfano anaendesha tipa hzi scania kwa kila route ana posho ya 3500 ikiwa mchana na usiku ni 5000. so daily yy hela ya kula anapata, ukizingatia amepata privilege kama bima bas anaweza asiguse mshahara kabisa.

K.N SOLANKI:- kila route trip town unapata 10k. if you are lucky ukiwa na deals unapata mizigo ya pembeni kwa wiki unatengeneza mpka 500k japo kwa magendo ila ni ya uhakika sana.

INTERPETROL; wanalipwa kwa USD ila ni parefu nasikia

USHAURI; kazi ya udereva pesa unapata lakini ni ngumu sana mkuu, inahitaji ulijue hustle mkuu na kua mjanja sana. kazi zake kupata ni kuhonga na magumashi kibao,.. ila when u gor for it atleast strive for large companies especially za mafuta hutajuta sana.. au kwa bakhresa , azania hvi atleast mambo c mabaya sana huko..



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…