Mshahara wa Januari vipi mbona unachelewa?

Hongera sana.
 
Mkuu wangu nakusihi sana usifanye Top up, kama unahitaji pesa bora ukope Bank ingine kwa hilo ongezeko la mshahara. Top up itakufilisi vibaya sana.
Samahani kama nitakua nimeingilia uhuru wako
Upo sahihi.
 
Shukrani,nimewaelewa.ahsanteni sana,Bora nivumilie tu au nikalianzishe kwingine,
Maana Nina
CRDB
PBZ next I think it will be this Kenyans bank,I don't exactly remember the name of this bank.
Nimesikia hii msg nimecheka sana! Mkuu kwanini mikopo mingi namna hiii mkuu? Huna SACCOS ukope huko? Banks Kiukweli makato Yao ni makubwa! Unaweza kopa 2m ukatumia muda mrefu kulipa na ukaumia sana! Enewei KAKOPE
 
Wakuu, huu ndo mfano halisi wa kujitia umasikini kupitia Top Up.
Angalia hapa chini mahesabu ya jamaa mmoja alikua na mkopo wa M 29 akataka Top up, ambapo kwa mshahara wake kikomo cha mkopo wake ni M 35.

Sasa aka Top up, kwa kupewa M 5.2 alafu Deni likasoma M 58 kwa miaka 10 yaani deni likaongezeka mara 2 ya lile deni la awali la M 29 tena kwa miaka 10 mbele alafu wewe unapewa M 5.2
 

Attachments

  • IMG-20250721-WA0011.jpg
    98.4 KB · Views: 29
Wamemuibia tu! Wahuni
 
Topup ni kama wizi wa kutumia silaha. Topup inafaa ikiwa settlement amount ni chini ya milioni sita
 
Top up kaelewane na loan officer bank macho kwa macho.

Sema braza top up sikushauri, bora huo mkopo uishe ue unachukua wa mwaka.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Kuna watu hatuna option zaidi ya top up ila kama ana option nyingine top up sio mpango
 
Anaejua ukitaka kufanya calculation ya top up unafanyJE KWENYE ESS.MFANO ULIKOPA 2M UMELIPA SEVEN MONTH UNATAKA UTOP UP,
WENYE KIJUA TUPIGANE TAFU
Kuliko ufanye top-up ni bora ukope upya bank nyingine kwa muda huo huo unaotaka. Huwa tunawala pesa zenu nyingi kwenye top-up. Hii siri hakuna loan officer wa bank uliyokopa utaenda akakuambia ukweli.
Mara nyingi watu wanaofanya top-up huliwa million 2-10 kulingangana na mkopo anaotaka. Hizo pesa ungezipata endapo ungechukua mkopo fresh kutoka bank nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…