elixer of life
JF-Expert Member
- Dec 10, 2016
- 635
- 630
Mimi ni muajiriwa katika sekta ya afya, idara ya pharmacy. Mnamo mwaka wa 2019 nilipata mashauri ya kinidhamu, kesi ilienda ikifikia hukumu nilipewa barua ya kulipa fedha mfululizo miaka mitatu, ila kiukweli maisha yalikuwa magumu. Hivyo nilianza kuomba msamaha kwa mkurugenzi, hatukupata majibu kutoka kwake, ila kwa mwaka 2022 nilianza kuona tofauti ya mshahara na hati yake.
Lakini tulipofika ofisi za utumishi hakuna msaada tuliopewa, kwani hati ya mshahara haikuonesha tena kipengele cha mashauri ya nidhamu, ila pesa ya basic salary ilionekana kupungua na pesa ya take home ilishuka kiasi kwamba walivyotuambia utumishi tulipe pesa ambayo inaonekana inachukuliwa bila maelezo ya salary slip, kwa upande wangu niligoma.
Tulikuwa wawili kwenye kesi, September 2022 walitufungia mshahara. Kiukweli nilipigana sana hadi ofisi za wazee nilifika, baadhi ya maafisa utumishi walituambia kuna wafanyakazi wenzenu wameleta majina yetu ili tuwafukuze kazi. Kichwa kiligonga kiukweli.
Sasa cha ajabu na kushangaza, sasa hakuna stahiki nilizopewa na salary slip hazina kipengele kilichokuwa kinataka pesa kwa ajili ya kulipa upotevu wa dawa. Binafsi hapo nyuma first appointment cheo changu kilikosewa toka TAMISEMI na nilipambana kubadili ila wapi, ikabidi nifanyie kazi cheo ambacho sio changu wala sijasomea kwa miaka sita. Niliambiwa nikimaliza mashauri ya kinidhamu nitapewa stahiki, lakini wapi, hadi leo nipo nyumbani kwa ugonjwa wa uongo ambao sina.
Kama kuna mtu anajua namna ya kutatua hizi shida inbox nipate haki zangu. Hadi sasa sina imani na eneo langu la kazi sababu nilipewa na vitisho pia.