It is fair and fundamentally right. Ronaldo ni mburudishaji, mamilioni ya watu wanapata faraja, furaha na hata kuongeza siku za kuishi kwa kutazama anayofanya uwanjani. Kuna uwezekano 30,000 kati ya watu zaidi ya 80,000 wanaoijaza Santiago Bernabeu wanaenda kumuangalia Ronaldo. Mamilioni ya jezi zinauzwa duniani kwa sababu zina jina la Ronaldo. Haya David Cameroun akaweke suti zake sokoni tuone watu wangapi watanunua.
Zaidi ya hayo pesa anayoipata Ronaldo anaitumia kufanya mambo yake yote ikiwemo msururu wa watu ambao mishahara yao inatokana na mapato ya Ronaldo, wakati David Cameroun anafanyiwa kila kitu na serikali, hana hata mtu mmoja anaesubiri mshahara kutoka kwenye mapato yake.