Sasubi Zabron
New Member
- Jun 21, 2024
- 1
- 1
1. Kukuza thamani ya pesa ya Tanzania
2. Kubadisha mfumo wa elimu ya Tanzania
3. Kulipa madeni yote ambayo Tanzania inadaiwa
Kivipi haya yote yatawezekana serikali ya Tanzania inatakiwa kujenga Shule maalumu ambazo zitatumia mifumo mipya tofauti na Ile ya zamani ambayo mtoto ili amalize masomo yake mpaka chuo Kikuu anatakiwa kusoma kwa miaka zaidi ya kumi na mitano ambapo mtoto huyo huyo kama akimaliza miaka yake Saba ya mwanzo anakuwa hajui kitu kuhusu maisha Kuna wengine wanamaliza miaka yao kumi na moja Shule lakini wakifika mtaani hakuna kitu wanajua.
Kwahiyo kuliko kupoteza muda mwingi shuleni na kuambulia akiri za darasani tu ni bora serikali ibadilishe mfumo wa utoaji elimu wake kwa kujenga Shule zenye mfumo wa mafunzo wa sekta mbalimbali ambazo mtoto anaanza kujifunza toka mdogo kama ni Shule ya mambo ya udaktari , michezo, sanaa, Uwalimu, uuguzi, uaskari, uanajeshi, ukulima, upishi, Uandishi wa Habari , mambo ya siasa, uanasheria, mambo ya uchumi, mambo ya Kodi, na sekta zote zenye Umuhimu kwenye nchi yetu watoto waanze kujifunza kuanzia darasa la kwanza hayo mambo na miaka isiwekwe mingi kama iliyowekwa sasa na hapo nyuma.
Hii itawasaidia Sana watoto kuwa wabobezi wa sekta tofauti tofauti na pia itakuwa ni rahisi Sana watanzania kusajiliwa kiurahisi hata kwenye mataifa yenye mipaka ya umri kwenye utoaji wa ajira, na itasaidia kutangaza nchi yetu kwani si tu kuwa hizi Shule zitakuwa zinafundisha watanzania tu bali Tanzania itakuwa inapokea watoto wengi kutoka mataifa mbalimbali kuja Tanzania kupata elimu.
Wageni wakiwa wanazidi kuingia nchini kwaajili ya kupata elimu pesa ya Tanzania itaanza kuwa adimu Sana kwani wageni watakapo zidi kuingia Tanzania watalazimika kubadilisha pesa zao kwenye benki Kuu ya Tanzania ili wapate pesa za Tanzania jambo ambalo litapelekea Pesa ya Tanzania kuzidi kupanda thamani kutokana na matumizi yake kuongezeka kwa kasi kwenye upande wa wasomi wa nje watakavyozidi kuingia nchini pia watalii watakavyokuwa wakizidi kuingia nchini Tanzania.
Kupitia faida itakayokuwa ikipatika kwenye ufundishaji wa watoto watakaokuwa wanakuja kutoka nje ya nchi pesa hiyo itatumika kulipia madeni ambayo Tanzania inadaiwa pia pesa itakavyo zidi kuingia Tanzania itaweza kuwekeza pesa kwenye nchi tofauti tofauti na kuzidi kufanya maboresho zaidi kwenye sekta mbalimbali nchini ili kuwaandalia mazingira taifa la kesho.
Upande wakulipa ada kwa watanzania iwekwe bei ambayo haita muumiza mtanzania ili watanzania waweze kunufaika zaidi na elimu iliyoanzishwa nchini kwao na kwa upande wa wanaotoka nje ya nchi wawekewe ada tofauti kulingana na nchini kwao wanavyolipia hii itawasaidia Sana kuendelea kukuza thamani ya Pesa ya Tanzania.
Eneo ambalo Tanzania inatakiwa kujenga hizo shule ni mkoa wa Mbeya kwani mkoa huo una ardhi ya kutosha pia kwenye upande wa vyakula ni mkoa uliobarikiwa zaidi hatakama serikali ikaamua kulima vyakula vya shule ili kupunguza gharama za manunuzi ya nafaka na kuepusha uadimu wa chakula nchini hii njia itasaidia kufanya ivyo.
Pia kupitia jambo hili Tanzania itatoa fursa tofauti tofauti kwenye upande wa ajira kwani shule zitakazo jengwa zitahitaji wafanyakazi kwenye upande wa ufundishaji, ufanya usafi, upishi, ulinzi , uuguzi na ulezi kwahiyo serikali italadhimika kutoa ajira ndani na nje ya nchi ili kupata walimu Bora zaidi na wafanyakazi Bora zaidi.
Kutakuwa na maswali mengi zaidi kwenye upande wa wale waliokuwa walimu wa mfumo wa awali itakuwaje kuhusu ajira watafukizwa au itakuwaje? Jibu ni kuwa hawatafutiwa ajira zao , watachukuliwa na kupatiwa mafunzo ya mfumo mpya na kila mmoja ataajiriwa kulingana na yeye uwezo wake wa kufundisha upo vizuri kwenye sekta ipi.
Maswali yatakuwa vipi kuhusu wanafunzi waliopo kwenye mfumo wa zamani itakuwaje? Jibu ni kwamba kwa wale wote ambao wapata elimu ya sekondari watalazimika kumaliza elimu yao kwa mfumo uliyokuwa ukitumika zamani pia kwa upande wa wanafunzi wa kidato Cha Tano, sita mpaka chuo nao watatumia elimu Ile Ile ya mfumo wa zamani ili kutokuwachanganya Sana kwa kile walichojifunza mwanzo ila mfumo mpya utaanzia kwa wanafunzi wa shule ya msingi elimu yao ya darasa la Saba ndio itakayo waelezea wao wanatakiwa kwenda kujifunza mambo ya sekta gani.
Kutakuwa na maswali mengi wapi serikali itapata hizo Pesa za kufanya mabadiliko hayo ? Jibu ni kuwa serikali inavyanzo vingi Sana vya kupata Pesa kwahiyo sioni kama kutakuwa na ubaya wa Pesa zilizopo kwenye mifumo ya serikali kutumika kuendeshea jambo hili pia hata kama serikali italadhimika kukopa pesa tena si vibaya ikope tu kwani kupitia mkopo huo ukifanikisha kuikamilisha shule hizo Pesa itakayopatikana itatumika kulipia madeni ya mwanzo na deni hili litakalochukuliwa sasa ambalo litakuwa ni deni la mwisho kwa serikali ya Tanzania kuchukua.
Tanzania tunayoitaka miaka mitano ijayo mpaka miaka ishirini na tano na kuendelea tunataka iwe ni nchi yenye uchumi mkubwa na kutotikiswa na nchi yeyote, wasomi wengi na wabobezi wa sekta tofauti tofauti, nchi isiyo daiwa bali iwe ni nchi yenye kuwekeza na kudai mataifa mengi, nchi yenye nguvu kubwa, nchi yenye amani na furaha, na nchi isiyo kuwa omba omba ndani ya Afrika na duniani kwa ujumla na hayo ndiyo maoni na maono yangu kwa serikali yangu ya Tanzania na kama hii insha haitashinda na kutofikishwa kwa serikali yangu basi nitafanya mwenyewe na kama itashinda lakini serikali yangu haita fanya kile nimesema basi Mimi mwenyewe nitafanya maisha marefu kwangu na baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu Amen.

Upvote
2