Mshambuaji Thomas Ulimwengu rasmi Al Hilal ya Sudan kwa mkataba wa mwaka 1

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Mshambuaji wa Kimataifa wa Tanzania Thomas Ulimwengu, amekamilisha usajili wa kujiunga na timu ya Al Hilal ya Sudan kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Wakala wa mchezaji huyo Jamal Kisongo amesema sababu kubwa ya kumrejesha Ulimwengu barani Afrika ni kutokana na kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu, na pia bado alikuwa na matatizo kuhusu kibali chake cha kazi nchini Sweden.

"Tukumbuke amekaa miaka mwili hajatumika, na alikuwa na tatizo la kibali cha kazi kwahivyo ili arudi kwenye timu bora barani Afrika. Lengo ni kumrejesha kwenye kiwango kizuri na baada ya muda atarudi Ulaya", amesema Kisongo.

Kisongo amesema Al Hilal (inayoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya makundi), wamefanikia kumsajili baada ya kuwazidi dau Super Sport ya Afrika Kusini ambao pia walikuwa wakimuania.
 
Huenda ikawa safari Ulaya mwisho hapo. Kila la heri kurudisha kiwango chako
 
Alifanya maamuzi mabaya sana alipokataa kusaini mkataba mpya na tp mazembe
Kama aliona muda wa yeye kutoka Afrika umewadia hakuna ubaya. Naweza kumlaumu kwa kutochagua sehemu sahihi ya kwenda ambacho angekuwa juu zaidi hasa Ufaransa
 
Angeendelea na TP mazembe yake tu na jamaa wangemuuza kwa timu nzuri hapo baadae ili wapate faida sasa yeye akaalazimisha kuondoka na free transfer
Washauri wake hawakumsihi ipasavyo
 
Kutoka ughaibuni mpaka mafichoni? Nini shida aisee dah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…