Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Mshambuaji wa Kimataifa wa Tanzania Thomas Ulimwengu, amekamilisha usajili wa kujiunga na timu ya Al Hilal ya Sudan kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Wakala wa mchezaji huyo Jamal Kisongo amesema sababu kubwa ya kumrejesha Ulimwengu barani Afrika ni kutokana na kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu, na pia bado alikuwa na matatizo kuhusu kibali chake cha kazi nchini Sweden.
"Tukumbuke amekaa miaka mwili hajatumika, na alikuwa na tatizo la kibali cha kazi kwahivyo ili arudi kwenye timu bora barani Afrika. Lengo ni kumrejesha kwenye kiwango kizuri na baada ya muda atarudi Ulaya", amesema Kisongo.
Kisongo amesema Al Hilal (inayoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya makundi), wamefanikia kumsajili baada ya kuwazidi dau Super Sport ya Afrika Kusini ambao pia walikuwa wakimuania.