Mshana Jr, agent wa Shetani JF?

Mshana Jr, agent wa Shetani JF?

Akitumia elimu yake aliyoipata nchini Afrika kusini ya Budhisim...na mchanganyo wa vitabu mbalimbali vya kishetani...ujuzi wake katika meditation na ulozi...

Sasa amekua kinara katika mada zote za kishetani hapa jukwaani JF... Na kwa kuwa Jf kila mtu anavutiwa na mada hizi za kutisha na kustaajabisha...basi amepata wafuasi wengi akiwafundisha na kuwaelewesha na polepole kuwaelekeza namna ya kufanya...si tu katika meditation bali pia katika vitu hatari kama viapo vya damu,uzuri wa shetani,eti lucifer sio shetani...na mengine mengi ambayo amekua akiyatoa....

1) Kuweni makini na anayoyasema
2) Na muwaze na kuamua ni kwa faida ya nani mnajifunza haya
3) Mkajiulize je Mungu wenu anafurahia hayo?
4) Na kwann watu wengi mnaotaka sana kujua haya ni wakristu?
5) Muogopeni mno...anataka kuwapotosha imani yenu

Hayo ni maoni yangu..
Na mzizi mkavu
 
Humu JF watu kujifanya wanajua Kuhukumu wenzao, as if wanawajua,kumbe apart from jina feki na sura feki hamna chochote wanachojua,zaidi ya kuotea otea thread zao,mshindwe
 
maishapopote kwanza nikupongeze sana kwa kutoa dukuduku lako ikiwa ni mtazamo wako kwangu kuhusiana na mada zangu
Najua ni una mengi zaidi ya kuandika kunihusu mimi na mada zangu na mambo yote yanayohusiana nazo...nitapenda kuwa bega kwa bega nawe Katika kueleweshana na kujuzana kwa uwazi na kwa mifano stahili huku tukitumia nukuu na lugha za kistaarabu
Naomba ushirika wako wa Karibu Katika hili kwa manufaa ya jukwaa
hebu nisaidia kutuwekea link za hizo mada, mie mwenyewe nishatamani kufatilia kwa ukaribu na kila ukiweka unitag niweze kufatilia kwa Ukaribu, hayo mambo unayoongea ni tangu Enzi za Nabii Suleyman lol. kuwafahamu hawa mashetani na wafuasi wake hatujakazwa.
 
Ni maoni yako ahsante kwa kutujuza ila mwisho wa siku wote / wengi humu ni watu wazima tunajua baya na zuri...
....not true, watu wazima ndo wanaoingizwa chaka vibaya sana, afadhali watoto wakiamini Mungu huwayumbishi....
 
hebu nisaidia kutuwekea link za hizo mada, mie mwenyewe nishatamani kufatilia kwa ukaribu na kila ukiweka unitag niweze kufatilia kwa Ukaribu, hayo mambo unayoongea ni tangu Enzi za Nabii Suleyman lol. kuwafahamu hawa mashetani na wafuasi wake hatujakazwa.
cheki nae atakupa link zote...tena ulivyo mrembo...sekunde tu
 
hujanishawishi hata kidogo kutofuatilia threads za huyu jamaa. kwa ufupi namkubali sana na mmoja ya watu wanaonikosha kwa mada na maoni yao. vivaa Mshana Jr.
unaweza kutaja faida hata mbili tatu ukizopata kutoka kwake,
zaidi ya kukutia hofu na mwisho wa siku unaangukia mikononi nwa waganga wa kienyeji na kuishia kuwa mtumwa wa shetani.
 
ni kweli ila namna anavyozifichua hizo siri za huko kuzimu ni kama anawainspire na kuwafundisha wakifanye hicho ambacho anawaambia...he is the Trainer,and not a Trainee
huu ndio ukweli namna anavyowasilisha mada zake ukizitazama kwa undani utagundua lengo lake ni kuwashawishi wanaomfuatilia kuendelea kuwajaza imani za kishirikina.
 
unaweza kutaja faida hata mbili tatu ukizopata kutoka kwake,
zaidi ya kukutia hofu na mwisho wa siku unaangukia mikononi nwa waganga wa kienyeji na kuishia kuwa mtumwa wa shetani.
mkuu mbona povu jingi jingi?? nani kakwambia nikisoma mada za huyu jamaa napata hofu? nani kakwambia nimeshakwenda kwa waganga wa kienyeji kwakua nilisoma posts zake? mkuu umetumia kigezo gani kujua naelekea kua mtumwa wa shatani?
just a very little advice: you better learn to think positive. so kila msoma biblia ni mkristu!!
 
Binafsi namkubali sana Mshana Jr mitizamo yake hasa inayohusu uzalendo,Kama yupo hivyo atajua yeyevingawa kiimani tunaambiwa,chukua jema hata kama linatoka kwa shetani
shetani kama alivyo hana jema,
kutafuta jema kwa shetani ni kujidanaganya.
 
Humu JF watu kujifanya wanajua Kuhukumu wenzao, as if wanawajua,kumbe apart from jina feki na sura feki hamna chochote wanachojua,zaidi ya kuotea otea thread zao,mshindwe
mtoa mada katoa maoni yake na ushauri,
una haki ya kuukubali au kuukata
kiukweli binafisi nimemwelewa alichomaanisha muhimu kaa mbali na hizo mada za kichawi zinazohamasisha ushirikiana zitakupeleka motoni.
 
Back
Top Bottom