Wanabodi.
Tanzania ni nchi yetu sote Waislam, Wakiristo, na wasiokuwa na dini tunamshukuru Mungu kwa kutupa moyo wa subira kuishi kwa upendo na kuvumiliana na kuheshimiana watu wa dini zote na wasiokuwa na dini kuna kitu kinaitwa (Coexistence) ambacho watanzania tunacho tumepewa na Mungu.
Hizi takwimu ambazo zipo kwenye idara za serikali na katika taasisi za dini zimetolewa kwa faida ya nani kisiasa, kidini, kibiashara, kimaendeleo, hau faida zake zipi takwimu zenyewe ni hizi hapa...
Ofisi ya Waziri Mkuu inaonesha Wakiristo ni 45% - Waislam ni 35%. TBC1 wametangaza Wakiristo ni 52% - Waislam ni 32%. Bodi ya Utalii inaonesha Wakiristo ni 45% - Waislam ni 40%. Tovuti ya Wakatoliki (
RCNet) inaonyesha Tanzania kuna Wakiristo ni 44% - Waislam ni 34%.
Takwimu hizi zimekuwa zikitumiwa katika uteuzi na maamuzi na serikali.
Hapo utaona umuhimu wa swali la dini katika sensa.
Tunajifanya hatujali dini wakati sehemu zote hizo, pamoja na ofisi ya Waziri Mkuu, wametaja asilimia za Waislam/Wakristo.
Ujinga mmoja tunaofanya ni kumuona Nyerere kama mtume, na hotuba yake aliyosema kwamba hakujua namba ya mawaziri wake kwa dini imechukuliwa kama kukataa kuhesabu watu kwa dini.
Wakati huo huo dunia inabadilika. Nakubali kwamba kuna uwezekano wa namba hizi kuleta matatizo (rationale ya watu wanaosema wana nia nzuri kukataa swali la dini kwenye sensa ni kwamba wengine -let's face it, waislamu- watatumia figures za dini kuleta chokochoko). Kwa hiyo wanasema tusiweke swali la dini ili kusiwe na official government figures za idadi ya watu kwa dini.Ili kusiwe na chanzo cha chokochoko kama za Waislamu kuanza kutaka nafasi za juu/ elimu kwa quotas za dini.
This argument is wrong. Because it is based on a deception.Because it fears the truth.
Ni kama vile serikali inataka kutumia manipulation kuzuia watu kujua ukweli. Hesabuni watu, wekeni swali la dini tujue Tanzania ina Wakristo wngapi na waislamu wangapi.Ondoeni mgogoro usio lazima. Halafu mtu akileta ujinga wa kutaka nafasi za uongozi kwa misingi ya dini tutakataa.
Serikali ikikataa kuhesabu watu na kuweka kipengele cha dini, inapalia moto hizi tetesi kwamba inakandamiza waislamu. Inafanya mgogoro uwe mkubwa kuliko ulivyotakiwa kuwa.
Kama mtu anapanga kuleta chokochoko kwa kutumia namba za sensa, usipompa hizo namba ndo umempa carte blanche ya kufanya chokochoko hizo, na hata kumuongezea sympathizers.
Mimi huona vibaya sana ninapoangalia ramani za statistics na kukuta Tanzania katika vitu vingi sana iko under "Data Not Available". Sensa ni zoezi lenye gharama kubwa sana na linatokea mara moja tu kila mlongo. Kwa nini tusiweke hili swali la dini hata academicians wanaotaka kujua hizi habari katika reseraches zao (kwa mfano, kama mtu anataka kujua relationship between religious belief and family planning/ reproduction rate ili ku shape government policy, atashindwa kupata reliable government figure.
Ile argument ya Nyerere ambayo imekubalika sheepishly, kwamba serikali hailazimiki kuhesabu watu kwa dini kwa sababu haijengi misikiti iko outdated, na pengine iliweza kukubalika nyakati zile tu kwa sababu Nyerere alikuwa strongman na watu walikuwa bado hawajaweza kum challenge vizuri. Na hata yeye inawezekana kabisa alikataa kuhesabu watu kwa sababu za political expediency zilizo les benevolent kuliko alivyotaka ionekane.Kwa sababu habari ya kujua idadi ya watu kwa dini -unless you are simpleton, and Nyerere was no simpleton- itakusaidia kwa mambo mengi zaidi ya kujenga misikiti, this is a simplistic approach.Nimetoa mfano hapo wa research ya kuangalia relationship between religious belief and reproduction rates, hii inaingia moja kwa moja katika government policy.
Sasa tunaweza kushindwa kuwa na the right government policy kuhusu reproductive health simply kwa sababu tume ignore umuhimu wa kuwa na government statistics (from a reliable source such as the census as opposed to from a religious body which is not above being prone to inflating figures).
Kuna siku watu watakaa na kucheka sana hii nchi ilivyokuwa inaendeshwa. In so many ways bado tupo katika Ujamaa unaoenda kwenye Ukomunisti. Ule unaokataa kuwepo kwa dini, kwa sababu unataka kumfanya kila mtu aamini kwamba serikali ndio dini pekee.
Bora ukweli mbaya (kujua idadi ya watu kwa dini, hata kama kuna uwezekano wa habari hii kuleta matatizo) kuliko uongo mzuri (kwamba Tanzania serikali haijali kabisa mambo ya dini na hivyo haina haja ya kujua idadi ya watu kwa dini).