SoC02 Mshangao katika haki

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Aug 22, 2022
Posts
7
Reaction score
3
UTANGULIZI
Neno 'HAKI' ni changamani ambalo linahusiana na namna ambavyo mtu anapata jambo analostahiki bila ya kikwazo chochote, na neno 'MSHANGAO' Linamuangazia mtu ambae ameshindwa kuamua baada ya mawazo yake kushindwa kuthibitisha baina ya vitu viwili ambavyo kuaminika kwake ni vigumu au tunaweza kusema 'Kupigwa na butwaa'

Yawezekana watu wengi hasa wale wa 'Ulimwengu wa tatu' tunashindwa kutofautisha na kutambua haki zetu na wajibu wetu, kama hiyo ni ndoto basi hata yale makosa yaliyozungumzwa hadi kwenye maandiko matukufu kama 'KATIBA' vipi tushindwe kuyatekeleza? Makosa ambayo kuyatenda kwake hata sheria hutetereka na haki kuvunjika, aliyemo hutoka na kuingia asiyekuemo, walioshuhudia wakageuka vipofu na kushindwa kuziba ufa ambao hupelekea ukuta wa 'HAKI' kuanguka.

Kama hiyo haitoshi, Wale wajuzi wa sheria hutia kwapani ujuzi wao na kauthiri wasiojua na hata Makonda na Madereva wa daladala wakawa ni wazazi wa Abiria ambao walistahiki kuwafariji Makonda na Madereva hao.

Ajabu ya wa wale waitwao Wasemaji husema mambo bila ya kujali mazingira, Wahusika, Aina za Wahusika, Mada ya mazungumzo yao na hata ukiwasikiliza unashindwa kufahamu nini lengo la Mazungumzo yao.hapa ndipo tunapopata 'MSHANGAO KATIKA HAKI'.

MALENGO YA ANDIKO
Andiko hili litaangazia masuala mbali mbali yanayohusu jamii ambayo kutokana na mambo kadhaa inaonesha 'MSHANGAO KATIKA HAKI' Mambo hayo ni kama vile Matumizi sahihi ya mitandao na wamiliki wa mitandao ya simu, Namna ya uchukuaji wa Abiria kwa Madereva na Makonda, Vikosi vya usalama, na namna mahakama zinavyoamua kesi.

Namna ya Uchukuaji wa Abiria. Katika suala hili, Haki inaonekana zaidi kwa Abiria ambao huonekana ni wahitaji zaidi wa 'HAKI' Kuliko Makonda na Madereva.Mfano Abiria anaweza kusimamisha gari popote na gari ikasimama kwa kustahiki au laa, lakini utata unakuja sehemu za kushushia Abiria hao hutaka kushushwa sehemu yoyote ambayo watakuwa wamefika safari yao bila ya kuzingatia sheria na taratibu huku wakisimamia kwamba ni 'HAKI YAO' hali inayofanya Madereva na Makonda wakose 'HAKI' Kwani makosa yote ya usalama huwakumba wao na hii hupelekea kuonekana wavunjaji wakubwa wa sheria.

Je! kupanda gari ikiwa imejaa kwa Abiria anayejua idadi ya Abiria wanaostahiki kuingia katika gari hiyo ni HAKI Kwa Madereva na Makonda?.


Matumizi ya mitandao ya kijamii. Suala la matumizi ya mitandao ya kijamii linafanya jamii iwe na Mshangao katika suala la HAKI, mfano wa mitandao hiyo ni instergam, feacebook, n.k. kupitia mitandao hiyo tunaweza kusema sasa imekuwa ni mahakama ya kushitaki maisha ya watu maana kumekuwa na vijiji katika mitandao ya kijamii ambapo maisha yote yamehamia huko.

Ni huko huko ambako watu wanapika na kula, mimba zinabebwa na kuzaliwa na ule upepo wa picha zisizo na maadili hasa kwa jamii ya Tanzania ndio kwao, maisha yakutengeneza, na hadaa za maumbo na pesa ambazo chanzo chake kukitambua ni vigumu, Watu huzalilishwa bila hata kujipanga na matokeo na kukabiliana na athari zinazoweza kuwakumba, wengine hupata dosari na kuonekana wabaya wao na matendo yao.

Je! Wamiliki wa mitandao hawaoni? Na hawana uwezo wa kuzuia kama wanavyozuia vifurushi waendeshaji wa mitandao ya simu? Hapa ndipo tunaona wazi kuwa kuna 'MSHANGAO KATIKA HAKI'.

Uamuzi wa kesi. Cha ajabu ni kwamba katika uamuzi wa kesi nako kuna 'MSHANGAO KATIKA HAKI' Eti si ajabu Hakimu aliyeaminiwa kupewa Rushwa ambayo inaweza kupoteza HAKI ya Mtendewa na kumpa faida mtendaji hali ya kuwa anahitaji kupata hasara.

Dhulma, unyang'anyi, kucheleweshwa kwa kesi ni 'MSHANGAO KATIKA HAKI'
Kama ningeulizwa kitu gani kinauwa HAKI ningesema Mahakama zetu zinachangia pakubwa sana.

Wasimamizi wa sheria na usalama Barabarani. Hili nalo ni zito sana kulitambulisha kwani linaleta 'MSHANGAO KATIKA HAKI' Wasimamizi wa Sheria na usalama barabarani tunaweza kuwaita wasodhambi ambao hujivika vilemba na majoho ya utukufu na hubadilika kulingana na mazingira. Hawa ndio wale wanaozitia mifukoni zile 100 na 200 ambazo hizo barabara hutegemea pesa hizo kujengwa.

Pato la taifa hulipoteza kwa njia labda zingelikuwa zimezibwa basi pato hilo lingetumiwa milele na milele.

Hapa Madereva na Makonda hukosa HAKI Kwani wanachokitowa hunufaisha wachache tofauti na mategemeo yao.

HITIMISHO
Haki inapokosekana dhuluma, uonevu, unyanyasaji na ukandamizaji huota mizizi ambayo ni athari kwa vizazi vilivyopo na vya baadae.

Habibu hamadi haji.
Habybuhaji@gmail.com
 
Upvote 1
Katika suala la mitandao ya kijamiii,mamlaka husika lazima iangalie tena sheria za mitandao ili kuwabana wanaopotosha maadili ya mtandao...hapo ndipo haki itapatikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…