Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Elon Musk, mshauri mwandamizi wa Rais wa Marekani, Rais Trump, amtaka bosi wake huyo kumpa msamaha muuaji, Derek Chauvin, mweupe, aliyekuwa na cheo cha afisa wa polisi nchini humo.
Elon Reeve Musk ni tajiri mkubwa anayemiliki kampuni za Tesla, Inc., SpaceX, na Twitter, na pia ofisa mwandamizi katika serikali ya Marekani kama mshauri mwandamizi wa Rais Donald Trump.
Mnamo Mei 25, 2020, Chauvin, mweupe, alibana shingo la George Floyd kwa goti kwa karibu dakika tisa akiwa amefungwa pingu na kulazwa uso chini mtaani, akilia "Siwezi kupumua"
Picha za muuaji huyo zilisambaa duniani zikimuonesha mtu mweusi aitwaye George Floyd akikata roho huku muuaji akionekana kutojali hata pale alipopigwa picha na mashuhuda wa tukio hilo!
Mapema mwaka 2021, Chauvin alishtakiwa kwa mauaji ya kiwango cha tatu, na mauaji ya kiwango cha pili ya Floyd mbele ya jopo la majaji mahakamani huko Minnessota, USA.
Mnamo Aprili 20, alihukumiwa kwa mashtaka yote na Juni 25, alihukumiwa kifungo cha miaka 22+1⁄2 gerezani pamoja na uwezekano wa kuachiliwa baada ya miaka 15
Kweli hujafa hujaumbika, huu ushirika wa watu hawa wawili Marekani unaweza kuwekewa LUKU na Wamarekani wenyewe tu na si kelele za dunia hata zikiungana kwa pamoja.