Mshikaji wangu ameanza kucheza forex, kila siku anauza vitu kidogo kidogo

Status
Not open for further replies.
Wasaidieni wenzenu karibu watawaweka rehani wachumba zao!!
Watanzania wenye moyo huo labda wachache mkuu. Unamwambia mtu akufundishe hiyo kitu ila kwa muda huo huna kiasi hiko chote kwa ajili ya mentorship, lakini anakutolea nje. Na huyo mtu daily unakuta post za screenshots za dollars. Binafsi naona hatuna nia ya kusaidiana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakupata Mwalimu mzuri tu
Pia hakupata kanuni nzuri tu
Lakini Pia Alijazwa upumbavu kama kupitia forex atavuna mamilion daily
Akae Chini ajipange upya
then inahitaji mda kufanya analysis Forex nikama kazi zingine usipokuwa na vigezo nikubeti tu
 
Watu wanapaswa kufahamu kuwa Forex ni tofauti kabisa na hizi network marketing kama foreveriving n.k. Hakuna kumleta mtu na mtu amlete mtu. Hii ni biashara kama ya beuro de change sema tuu yenyewe unakua online wakati yale maduka yanakuwa physically.
Forex ni biashara kama biashara nyingine , kuna kupata faida na wakati mwingine kupata hasara kama mambo yakienda vibaya. Kwa msingi huo niwaulize ni biashara gani ambayo mtu hutegemea faida tuu bila kufikiri kua pia kuna uwezekano wa kupoteza. Wangapi wanapoteza ktk biashara ya tikiti, wangapi wanapoteza ktk biashara ya nafaka n.k. Sasa kwa nin mtu akipoteza ktk biashara ya Forex inakua nongwa?
Forex ndiyo soko kubwa kuliko yote duniani ambapo daily turn over yake ni takribani dola trilioni tano. Taasisi kubwa na mabenki duniani znafanya biashara hii. Retail traders kama mimi na wewe tuna mchango mdooooogo sana ktk forex almost negligible. Volatility ya soko ndo itakupa faida kama soko likienda upande wako and vise versa.
Ndugu watanzania najua sisi ni wavivu saana kusoma, lakini nivema kasumba hii itutoke tujifunze vitu kabla ya kufanya siyo mara umekimbilia kulima mpunga, tikiti, mara umekimbilia ku tradr forex bila kusoma ukaijua ki undaaani kabisaa.
Halafu syo kila biashara kila mtu ataiweza au ataipendeza, kuna wengine wanapenda kuuza mtumba , wengine mafriji na wengine ku trade forex ndo wanapenda na ni vyema kufanya ukipendacho na usimdharau afanyae usichokipenda maana mwisho wa siku ni mkate ukae kwenye meza. Mimi siyo mkufunzi wa forex lakini ukitaka nitakuelekeza wapi ukasome maana maatifa ni kitu cha muhimu saana hata kama usipotaka kuwa trader lakini kujua vitu ni muhimu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…