Mshikaji wangu ameanza kucheza forex, kila siku anauza vitu kidogo kidogo

Status
Not open for further replies.
Huyo Adam Khoo hata mimi namuangaliaga yuko vizuri saana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Thank God nimepitia thread yote nimemaliza
Kuna tatizo watanzania hatuna udadisi wa vitu ambavyo tunajidai tunavipenda
Enzi zetu zile kulikuwa na watu ni wapenzi wakubwa filam za James Bond lakini ukiwauliza real name ya James Bond anaitwa nani hawawezi kukwambia the same applied kwa wapenzi wa Mr, Bean
Mimi nimeona watu wengi humu wana urge humu lakini ile tuu kuupitia huu uzi wote word to word wengi wao hawajadiriki
Mimi mwenyewe ni Muhanga wa hili nimekaa kwenye sector ya fedha zaidi ya miaka 18 lakini sikuwahi kudiriki kutaka kujua kama kuna dunia nyingine ya Online Forex Trading
Niliwahi kufanya manual trading kwenye DSE nisiseme uongo mimi ni miongoni mwa watu wachache tuliopiga pesa nzuri kwenye IPO ya Twiga, NICO na UTT lakini niwaambie ukweli 90% ya waajiriwa walioko kwenye sector ya Fedha ni weupe saana
Nilichogundua ktk jamii zetu kuna mambo ya kutishana sana na mtu anakutisha ktk kitu ambacho yeye mwenyewe hakijui
Siku 4 zilizopita nimekutana na Dogo mmoja hapa Dubai ndio ameanza kunitoa tongo tongo. Na ktk siku hizo 4 mimi ni kujichimbia kwenye YouTube kwa kweli kuna hazina kubwa ya Elimu humo nimekutana na Adam Khoo. Na hapo ndio nilipogundua tatizo jingine kwamba mtu kitu unakipenda lakini hutaki ku dedicate muda kwa ajili ya kukifanyia utafiti, wengi tunapenda blah blah za humu JF udandie issue katikati uanze kukomenti, kubisha, kutukana na kadhaalika. Hayo nimeyaona leo humu humu JF kwenye thread iliyokuwa inahusu Hydroponic Fodder Systems ni thread ambayo ilikuwa na posts takriban 650 lakini unaona kabisa watu wanauliza silly questions kiasi kwamba angesoma posts 100 zilizopita angeweza pata jibu sahihi

Ktk siku 4 zilizopita niseme ule ukweli najuta kwanini sikuijua mapema Forex
Na uzuri wenyewe wanatahadharisha watu wasiingie na mentality kwamba unaingia kwenye biashara ya kuwa Milionea haraka haraka kuna misingi yake na ukiangalia kwa undani hii ndio misingi ya biashara zote Duniani nayo ni :


Keys to be Big Trader in Forex

1. Consistency
2. Discipline
3. Confidence
4. Patience
5. Passion





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana na karibu chamani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hii forex nilianza kijifunza kazi na ratiba zikabana nikaacha kwanza natafuta mda nijifunze tenaa
 
Kinachofanya wengi kufail katika forex trading ni ile mentality ya GET RICH QUICK. Watu wanaaminishwa na matepeli wa forex kwamba forex ni kupiga hela tu tena fasta fasta. Wanawapa elimu ya uongo na kweli ya siku mbili tatu (forex basics) lakini nyuma ya pazia hawa trainers wanakuwa na mission ya kupiga hela kupitia hao wanafunzi wao. Mwisho wa siku hawa wanafunzi wa forex waanza kutrade live na kuambulia kipigo cha mbwa koko na mwisho wa siku wanaichukia na kuona kwamba forex ni kama utapeli. Ni kweli kwenye forex kuna hela kama utakuwa na hayo uliyoyasema. But namba 1 . ni Elimu sahihi ya forex na kuipenda hii business. Upendo (passion) juu ya jambo lolote huleta nguvu za ajabu za kulifanya hilo jambo hata kama litakuwa gumu kiasi ganai!
 
Unateseka na forex we jamaa, utafikir umetukopesha mitaji
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui kama walikuelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atakuwa amefungua Forex wallet, na wanamhifadhia vitu vyake online, acheni majungu na wivu nyie watu. Fursa za Forex ni nyingi na nyingi ni za kampuni yenyewe.
 
Bado sijaona tajiri halisi mbongo kwenye hii biashara, watatoka mabilionea wachache Sana sababu the business is real na haiaminiki[emoji3] , mabilionea tutabaki kuwa wachache mno sababu utajiri ni imani ,
Umeshindwa kuiamini forex, amini utajiri wa makete njombe basi[emoji38][emoji38][emoji38]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poor mentality! Kwani wafanya biashara wote ni mabilionea? Forex ni biashara kama zilivyo biashara nyingine hivyo kila mtu anafanya hii biashara kulingana na targets zake. Siyo kila anayefanya biashara lazima awe bilionea hayo ni mawazo pori na nakuomba uyaondoe kichwani mwako!
 
Fact
 
Kwa watumiaji wa TemplerFx Tuma email hii sasa bila kuchelewa"tuma email kwenda support@templerfx.com,andika ivi please make my account under the agent 123796 my account no is andika no yako ya account ya mt4 bila password.Spread the Love. kwa maelekezo zaidi nicheck +255767913761(whatsapp only)
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…