Mshikaji wangu anatembea na ex wangu

Mshikaji wangu anatembea na ex wangu

KIBUGAmk

Member
Joined
Jan 22, 2024
Posts
83
Reaction score
139
Kuna mshikaji wangu anatembea na ex Wangu ambaye nimeachana nae miezi 5 iliyopita, kiukweli huyo ex simpendi lakini mshikaji wangu ananiboa sana, ina maana alikosa demu mwingine mpaka aje kutembea na mashemeji zake

Naomba ushauri nimfanyeje huyu mshikaji wangu maana naona ni kama anasafiria nyota yangu😂😂 nilitaka nimkate mitama mbele ya huyo ex wangu ila basi tu sitaki kesi 😂😂
 
Usije ukamsusia mwanamke ambaye bado unampenda utakufa kwa presha. Kama ulifikiri atateseka na kurudi kukupigia magoti ulibugi mkuu. .Huyo rafiki yako atakuwa amemuonea huruma shemeji yake maana anajua fika wewe ndiye mmbaya shemeji hakuwa na kosa. Acha kumzibia x wako bahati inatakiwa uanze kumuita shemeji maisha yaendelee.
 
Sasa kama humpendi ex wako mbona unaumia ukiachana na mtu maanake maisha yake hayakuhusu kwa chochote hata umkute na nani kwakua mshafunga mahusiano .
Sio kwamba huyu mshikaji wang alikuwa akimtamani shemeG yake tangu kipindi nipo nae,? So kumuacha ameona ni fursa kwake
 
Ukikiona cha nini wenzako wanajiuliza nitakipata lini?
Usiache mwanamke ambaye bado una feelings naye.Mateso huanza taratibu.
 
Bado unampenda?

Kama humpendi acha kufuatilia maisha ya ex jamani!
 
H



Hapana huyu mshikaji wang kuna time hadi ananikera kuna muda ananiambia eti "" Oi nakuja hapo nyumbani kwako nipo na shemeG yako tunakuja kukusalimia". Huo si uchokozi kabisa[emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Hapo hua anamwambia kabisa demu wake twende ukamsalimie shosti yako Fj4family [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hapo urafiki ndio umeishia, ila ipo siku huyo ex wako atamwaga mboga zote utajua mengi wakiachana
 
Back
Top Bottom