mshike sana elimu usimwache......... Ebu shuka na haka ka stori.

mshike sana elimu usimwache......... Ebu shuka na haka ka stori.

shyja

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2013
Posts
410
Reaction score
63
***KUSOMA NI BURE***
Kuna MAJAMBAZI
walivamia BENKI KUU sasa
Jambazi akawaambia watu
waliokua mule ndani
"Wote laleni chini
atakaeinuka namsambaza
ubongo, Pesa ni za serikali
ila roho za kwenu"
wananchi woote wakalala
chini, SASA HII INAITWA
DHANA YA USHAWISHI
yaani kubadilisha njia ya
kawaida ya kufikiri!!
Kuna dada kwa woga wa
kuuawa akawa amelala
chini klmitego, JAMBAZI
likamwambia "Dada embu
kua na Adabu, chukua
kanga ujifunike hili ni
tukio la UJAMBAZI na si la
UBAKAJI. SASA HUU
UNAITWA WEREDI yaani
kuzingatia kazi moja ya
msingi iliyokupeleka
sehem husika!!
Walipotoka kwenye wizi
huo kuna jambazi mdogo
mwenye shahada ya
uzamili ya biashara
akamuambia mwenzake
"tuzihesabu hizi pesa" yule
mkubwa akamcheka kwa
dharau na kumwambia
"wewe ni mjinga hakuna
haja ya kuzihesabu, ikifika
saa mbili usiku
watatutangazia kupitia
vyombo vya habari kua
tumeiba tsh ngapi!! SASA
HUU UNAITWA UJUZI yaani
siku hiziujuzi ni bora
kuliko vyeti!
Huku benki nako meneja
akamwambia mhasibu kua
"jumlishe na zile milion80
tulizoiba, HUKU KUNAITWA
KUCHEZA NA CHAKI yaani
kuendana na tukio japo
baya kwa faida binafsi!
Mhasibu akafurahi sana na
kusema "dah wizi kama
huu ukiwa unatokea kwa
mwezi mara mbili ingekua
burudani mno" HUKU SASA
UKISIKIA KUA NA MAWAZO
CHANYA yaani furaha ndo
kitu cha muhimu zaidi!!
Meneja nae kafurahi sana
kwa kua sasa matatizo
yake yametatuka kwa
tukio la wizi, SASA HUKU
KUNAITWA KUTHUBUTU
yaani kutumia fursa
inapojitokeza hata kama ni
hatari kias gani!!
HAYA, usiku sasa taarifa ya
habari ikasema wizi
mkubwa umetokea benki
kuu na majambazi
wameiba milion 100,
majambazi kusikia hivyo
wakaanza kuhesabu zile
pesa lakini wakajikuta na
milioni 20 tu, Yule jambazi
mkubwa akasema "Dah
yaani Meneja kaiba mara
nne zaidi yetu bila hata
kutikisa msuli, aah bora
umeneja kuliko ujambazi,
HII SASA INAITWA ELIMU-
Ishike sana ina nguvu
kuliko bomu la nyukilia!!
 
ustaarabu unahitajika. Najua kuna watu wana degree za matusi. Ila kumbuka which goes arounda comes around.
 
Haka kastori katam sana mkuu... na ndio maana waswahili wanasema "Usilolijua ni sawa na usiku wa giza".....
 
Elimu iko juu zaidi ya yote.xnk 4 ur good story
 
Back
Top Bottom