Mshindi wa kwanza kuondoka na 30M (Vijana uchumi challenge)

Kibenje KK

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2016
Posts
284
Reaction score
442
Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana imeandaa Shindano la Vijana Uchumi Challenge lenye kauli mbiu ‘Wana tunafikiri, Taifa linasonga’.

Shindano hili linalenga kukuza Mawazo ya vijana, yenye ubunifu, yanayotekelezeka na endelevu katika kulinda na Kukuza Uchumi wa Taifa letu dhidi ya athari za misukosuko ya kimataifa.

Swali muhimu katika shindano hili ni;

“Inapotokea tishio la Uchumi wa Dunia kushuka kutokana na misukosuko ya kimataifa ikiwemo vita, ushindani wa kiuchumi na kiteknolojia, ni changamoto zipi zinazoweza kuikumba Tanzania; na nini kifanyike ili uchumi wa Tanzania uendelee kuimarika?”

Shindano hili linakaribisha ushiriki wa kijana yeyote wa kitanzania mwenye umri kati ya miaka 15 – 35.

Ili kushiriki, kijana mmoja mmoja anakaribishwa kuwasilisha wazo lake, kwa njia ya maandishi yasiyozidi maneno 300 au kwa njia ya video isiyozidi dakika 3 kupitia kiunganishi: hiki hapa chini 👇

Powered By Edodoso Forms

Link iko pia kwenye bio ya @orvijana

Kabla ya Tarehe 30 April 2026. Wazo linalowasilishwa ni sharti likidhi vigezo vifuatavyo ambavyo vitatumika kupata washindi:

1. Ubunifu: Kiwango cha fikra mpya na upekee wa wazo.

2. Uelewa wa Changamoto za Kiuchumi: Kiwango cha uelewa wa mshiriki kuhusu changamoto za kiuchumi za sasa na muktadha wa kimataifa.

3. Uhalisia: Utekelezekaji wa wazo na uwezekano wake kutekelezwa kwa vitendo.

4. Athari kwa Uchumi: Mchango unaotarajiwa wa wazo katika kukuza uchumi wa taifa.

5. Uwezo wa Kuleta fursa: Uwezo wa wazo kuzalisha na kuongeza fursa za ajira kwa vijana

6. Uendelevu: Uwezo wa wazo kudumu na kuleta matokeo chanya ya muda mrefu.

7. Ubora wa Uwasilishaji: Mpangilio, uwazi na urahisi wa kuelewa pendekezo.

Vijana Wote Mnakaribishwa.
 
Nch ya hovyo hii

Nenden pale udsm udom sua mzumbe kuna maprof na madaktar wameandika paper za aina hyo kibao ambazo zonahitaj implementation kuwa katika uhalisia lakn zipo katika makabat kwa ukosefu wa pesa kidogo TU

Toka ANAEJIITA RAHISI atoe maboko mna hangahika SANA

Wakat wa corona mbona uchum ulishuka na hamkuhtaj vjana waandike namna ya kujinasua?
 
Huu ndio UPUMBAVU wa kufikiri MOTIVATIONAL SPEAKERS wanaweza kuwa PROBLEM SOLVERS.

Huu UTAWALA wa huyu BIBI wanachojua ni WIZI, UFISADI, na MAUAJI tu.
Mbona hasira hivyo?
 
Hata wakiandika "Silikali" itafanyia kazi? (Implement)?
 
Ngoja niingie kwenye Kinyang'anyiro. Naanza na ideas za JF kwenye jukwaa la Stories of Change.

Sina muda wa kupoteza.
 
30ml sio , big deal.

Kuna uwezekano mkubwa wa mawazo ya hao vijana 100 yakawa yana tija kwa kupitia sekta mbalimbali za kiuchumi,

Sasa zile billions 200 ndio zitumike kutoa mitaji kwenye hizo sekta za vijana waliotoa mawazo Bunifu .

Uchumi wenye tija ni ule ambao ni distributed, Sasa kusema mawazo 3 Bora, sio kweli.

Kwa sababu uchumi Kuna vitu vingi vinategemeana
 
Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana imeandaa Shindano la Vijana Uchumi Challenge lenye kauli mbiu ‘Wana tunafikiri, Taifa linasonga’.

Shindano hili linalenga kukuza Mawazo ya vijana, yenye ubunifu, yanayotekelezeka na endelevu katika kulinda na Kukuza Uchumi wa Taifa letu dhidi ya athari za misukosuko ya kimataifa.

Swali muhimu katika shindano hili ni;

“Inapotokea tishio la Uchumi wa Dunia kushuka kutokana na misukosuko ya kimataifa ikiwemo vita, ushindani wa kiuchumi na kiteknolojia, ni changamoto zipi zinazoweza kuikumba Tanzania; na nini kifanyike ili uchumi wa Tanzania uendelee kuimarika?”

Shindano hili linakaribisha ushiriki wa kijana yeyote wa kitanzania mwenye umri kati ya miaka 15 – 35.

Ili kushiriki, kijana mmoja mmoja anakaribishwa kuwasilisha wazo lake, kwa njia ya maandishi yasiyozidi maneno 300 au kwa njia ya video isiyozidi dakika 3 kupitia kiunganishi: hiki hapa chini 👇

Powered By Edodoso Forms

Link iko pia kwenye bio ya @orvijana

Kabla ya Tarehe 30 April 2026. Wazo linalowasilishwa ni sharti likidhi vigezo vifuatavyo ambavyo vitatumika kupata washindi:

1. Ubunifu: Kiwango cha fikra mpya na upekee wa wazo.

2. Uelewa wa Changamoto za Kiuchumi: Kiwango cha uelewa wa mshiriki kuhusu changamoto za kiuchumi za sasa na muktadha wa kimataifa.

3. Uhalisia: Utekelezekaji wa wazo na uwezekano wake kutekelezwa kwa vitendo.

4. Athari kwa Uchumi: Mchango unaotarajiwa wa wazo katika kukuza uchumi wa taifa.

5. Uwezo wa Kuleta fursa: Uwezo wa wazo kuzalisha na kuongeza fursa za ajira kwa vijana

6. Uendelevu: Uwezo wa wazo kudumu na kuleta matokeo chanya ya muda mrefu.

7. Ubora wa Uwasilishaji: Mpangilio, uwazi na urahisi wa kuelewa pendekezo.

Vijana Wote Mnakaribishwa.
Vipi kuhusu mshindi

Vijana Wote Mn
 
Back
Top Bottom