Mshindi wa Pili wa BBA Hotshots 2014: Akanusha kupewa pesa na tajiri wa Nigeria

Mshindi wa Pili wa BBA Hotshots 2014: Akanusha kupewa pesa na tajiri wa Nigeria

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,016
Reaction score
2,195
Mshindi wa pili wa BBA Hotshots, Tayo kutoka Nigeria amekanusha ripoti zilisambaa wiki hii kuwa amezawadiwa $350,000 na bilionea wa Nigeria baada ya kuzikosa $300,000 za BBA zilizonyakuliwa na mshindi wa kwanza mwaka huu Idris wa Tanzania.

Tayo.jpg

Idris (kushoto) Tayo (kulia)

Ripoti hizo zilidai kuwa Tayo alipewa zawadi hiyo na bilionea aitwaye Ayiri Emani kama kifuta jasho au fidia ya kuzikosa $300,000 za mshindi wa HotShots.

Tayo amekanusha habari hizo alipohojiwa na kituo cha Radio 1 South Africa. Amesema kuwa habari hizo za kuwa amepewa kiasi hicho kikubwa cha pesa na huku hata hamfahamu bilionea huyo, zimemletea usumbufu kwasababu watu wengi watadhani yeye ni milionea na huku sio kweli.

Tayo aliongeza kuwa yeye na Idris ni marafiki na anatarajia kuja Tanzania mapema iwezekanavyo.

Chanzo: Big Brother Africa 2014
 
We are cheating again TZ,thanks muumba mbingu na ardhi,bado miss world banah,tupige kura please,download application kwenye smart phones chagua lugha kwa kubofya bendera ya england then piga kura kwa kuchagua washiriki watatu ukianza na happy wa tz,let's do it jamaaaaan we caaaaaaaan

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom