Mshindi wa Shindano la Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (JF Stories of Change) kujulikana Ijumaa tarehe 15 Oktoba, 2021

Mshindi wa Shindano la Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (JF Stories of Change) kujulikana Ijumaa tarehe 15 Oktoba, 2021

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Yule mshindi wa Shindano la “JF Stories Of Change” atakayejinyakulia kitita cha Tsh. Milioni 5 anatarajiwa kutangazwa siku ya Ijumaa Oktoba 15, 2021 katika hafla fupi itakayoanza saa 12 jioni mpaka saa 4 usiku.

Hafla hiyo ya kutangaza na kukabidhi washindi zawadi itaambatana na Chakula cha Jioni, Vinywaji na Burudani.


Kuhusu Shindano

Jamii Forums (JF) ilitoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye shindano la uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko (Stories of Change).

Shindano lilikusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye

Pia, shindano lililenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Shindano hili lilianza Julai 14 hadi Septemba 30


Zawadi kwa Washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-


Mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu Tsh. Milioni 5

Mshindi wa Pili atapata fedha taslimu Tsh. Milioni 3

Mshindi wa Tatu atapata fedha taslimu Tsh. Milioni 2

Zawadi nyingine zitahusisha Laptop na Simu za mkononi

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal)

Zaidi, soma; Mrejesho: Je, ulishiriki shindano la “JF Stories of Change?” Kaa karibu na PM yako
 
Upvote 41
Presha tunayoipataga wazee wa kubeti wacha na nyinyi washindani wa hili shindano muionje.

Yaani hapo ni sawa umeomba zitokee goli 3 na mpaka dakika ya 83 matokeo ni 1:0.
Hapo ndio unaamua kulala na kuandaa mkeka ujao.
 
Bora tupumue uko PM .matangazo yalikua mengi wana sumbua sana hawa washiriki
Kumbe hata shetani aliombwa kura? Nilidhani Ni Mimi tu.
Kama wataangalia wenye like nyingi hata wanyonge wataambulia japo laptop.
 
Back
Top Bottom