Mshindi wa Shindano la Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (JF Stories of Change) kujulikana Ijumaa tarehe 15 Oktoba, 2021

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Yule mshindi wa Shindano la “JF Stories Of Change” atakayejinyakulia kitita cha Tsh. Milioni 5 anatarajiwa kutangazwa siku ya Ijumaa Oktoba 15, 2021 katika hafla fupi itakayoanza saa 12 jioni mpaka saa 4 usiku.

Hafla hiyo ya kutangaza na kukabidhi washindi zawadi itaambatana na Chakula cha Jioni, Vinywaji na Burudani.


Kuhusu Shindano

Jamii Forums (JF) ilitoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye shindano la uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko (Stories of Change).

Shindano lilikusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye

Pia, shindano lililenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Shindano hili lilianza Julai 14 hadi Septemba 30


Zawadi kwa Washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-


Mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu Tsh. Milioni 5

Mshindi wa Pili atapata fedha taslimu Tsh. Milioni 3

Mshindi wa Tatu atapata fedha taslimu Tsh. Milioni 2

Zawadi nyingine zitahusisha Laptop na Simu za mkononi

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal)

Zaidi, soma; Mrejesho: Je, ulishiriki shindano la “JF Stories of Change?” Kaa karibu na PM yako
 
Upvote 41
Thanks, waiting interestingly!
 
Mmeshatangaza mshindi??

Kama bado tupeni vigezo mtakavyotumia kuchagua mshindi ili tujue mapema baadae tusije kulaumiana baada ya matokea.

Je JF haiwezi kumuongezea kura mtu wanayemtaka?
Je, JF haiwezi kumuongezea LIKES mtu wanayemtaka

Maswali uangu ni hayo tu, ntashukuru nikijibiwa kabla mshindi hajatangazwa
 
Ondoa hofu anza sasa niliupenda uzi waako daah haijaitwa na wewe
sijaitwa wala sijaona pm yoyote mpaka sasa labda kutokana na kura kuwa chache

ila najipa moyo kuwa niiondoe hofu nianze sasa ....... hahhaaaaaaaaaaaaaa

ni kitabu changu hicho kama utahitaji nakiuza tuwasiliane mkuu
 
hahhaaaaaaaaaaaaaaaa imenibidi nicheke ngoja watakujibu soon ondoa hofu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…