Mshindi wa Shindano la Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (JF Stories of Change) kujulikana Ijumaa tarehe 15 Oktoba, 2021

Mshindi wa Shindano la Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (JF Stories of Change) kujulikana Ijumaa tarehe 15 Oktoba, 2021

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Yule mshindi wa Shindano la “JF Stories Of Change” atakayejinyakulia kitita cha Tsh. Milioni 5 anatarajiwa kutangazwa siku ya Ijumaa Oktoba 15, 2021 katika hafla fupi itakayoanza saa 12 jioni mpaka saa 4 usiku.

Hafla hiyo ya kutangaza na kukabidhi washindi zawadi itaambatana na Chakula cha Jioni, Vinywaji na Burudani.


Kuhusu Shindano

Jamii Forums (JF) ilitoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye shindano la uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko (Stories of Change).

Shindano lilikusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye

Pia, shindano lililenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Shindano hili lilianza Julai 14 hadi Septemba 30


Zawadi kwa Washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-


Mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu Tsh. Milioni 5

Mshindi wa Pili atapata fedha taslimu Tsh. Milioni 3

Mshindi wa Tatu atapata fedha taslimu Tsh. Milioni 2

Zawadi nyingine zitahusisha Laptop na Simu za mkononi

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal)

Zaidi, soma; Mrejesho: Je, ulishiriki shindano la “JF Stories of Change?” Kaa karibu na PM yako
 
Upvote 41
Mkuu nikupe na hongera kwanza maana kufikisha hizo kura gumu ni mziki!! Hongera mkuu.
Ahsante. Mkuu tutulie aisee muda unakaribia tutamjua nani.mshindi hivyo tuache papara wakuu wapo huko jikoni wanapika mavitu muda kidogo wanatupakulia hapa jamvini kila kitu tutakiona tuwaamini
 
Jibu la nini tena KENZY hebu nikumbushe uzee huu nasahau mapema
Abrianna mama si nilikuambia naomba niwe wako!.. nipo radhi hata uninyonge lakini Mimi niwe nawe tu..😀
Mi kwako nimekufa nimeoza yani. Nakupenda mpk mbele sioni..😅
 
Ahsante. Mkuu tutulie aisee muda unakaribia tutamjua nani.mshindi hivyo tuache papara wakuu wapo huko jikoni wanapika mavitu muda kidogo wanatupakulia hapa jamvini kila kitu tutakiona tuwaamini
Yeah ndugu just be cool.

Mkuu unavyotumia wingi Sasa utafikiri namimi nilishiriki..😂
Mi ndugu naandikaga nyuzi za kuumizwa tu yani wadada wananichomolea mpk naitwa konokono..🤣
 
Sio mpaka ujifunze,wakati mwingine akili ikichoka inahitaji kurelax!Na ule uzi unaoffer aina flani hivi ya relaxation!
Zinaa na uchafu doesn't offer relaxation bwana zaidi ya wapenda nyeto kuipenda, nowdays dhambi zimekuwa sehemu ya relaxation mhhhhh!
 
Back
Top Bottom