Mshirika wa karibu Joseph Kabila Alexis Thambwe mwamba Akamatwa Kinshasa

Mshirika wa karibu Joseph Kabila Alexis Thambwe mwamba Akamatwa Kinshasa

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Aliyekuwa Rais wa Seneti na Waziri wa Sheria nchini DRC, Alexis Thambwe Mwamba amekamatwa asubuhi ya leo Ijumaa tarehe 23 Oktoba 2026 nyumbani kwake katika eneo la Macampagne Ngaliema jijini Kinshasa.

Thambwe Mwamba, ambaye ni mshirika wa karibu na nguzo muhimu ya kambi ya Rais wa zamani Joseph Kabila, amekamatwa katika oparesheni kubwa iliyohusisha upelekaji wa zaidi ya wanajeshi 30 nyumbani kwake.

Vyombo vya habari vya ndani nchini humo ikiwemo Actualite vimethibitisha kuwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80 amechukuliwa na vikosi vya usalama, ingawa sababu rasmi za ukamataji huo bado hazijawekwa wazi.

Seneta wa upinzani, Salomon Kalonda amelaani vikali ukamataji huo akitaja kuwa ni wa "ubabe na "uchochezi mkubwa" unaoonesha mwelekeo wa kiimla wa serikali hasa wakati huu nchi hiyo ikikabiliwa na migogoro ya kisiasa na mijadala ya kubadili Katiba.

ALEX.jpeg
 
Ila Africa tuna matatizo ya problem kwakweli. Yaani Serikali inahangaika na Mzee wa miaka 80 kweli? Tena kwa kupeleka wanajeshi 30 kumkamata? Halafu Wazungu wakimchora Shetani ana rangi nyeusi mnalalamika.
Maana yake kuna jambo
 
Aliyekuwa Rais wa Seneti na Waziri wa Sheria nchini DRC, Alexis Thambwe Mwamba amekamatwa asubuhi ya leo Ijumaa tarehe 23 Oktoba 2026 nyumbani kwake katika eneo la Macampagne Ngaliema jijini Kinshasa.

Thambwe Mwamba, ambaye ni mshirika wa karibu na nguzo muhimu ya kambi ya Rais wa zamani Joseph Kabila, amekamatwa katika oparesheni kubwa iliyohusisha upelekaji wa zaidi ya wanajeshi 30 nyumbani kwake.

Vyombo vya habari vya ndani nchini humo ikiwemo Actualite vimethibitisha kuwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80 amechukuliwa na vikosi vya usalama, ingawa sababu rasmi za ukamataji huo bado hazijawekwa wazi.

Seneta wa upinzani, Salomon Kalonda amelaani vikali ukamataji huo akitaja kuwa ni wa "ubabe na "uchochezi mkubwa" unaoonesha mwelekeo wa kiimla wa serikali hasa wakati huu nchi hiyo ikikabiliwa na migogoro ya kisiasa na mijadala ya kubadili Katiba.

Ukanda wa madikteta
 
The Democratic Republic of Congo likely will descend into anarchy once again the way it did immediately after independence from the colonial powers of Belgium.

The incumbent president Mr. Felix Tshisekedi is riding a tiger in the country and prodding to seek the unconstitutional extension of his mandate so as to reign past the 2028 election which he is constitutionally barred from running.

If he manages to jump the gun and amend the constitution so as to contest for the third term it's obvious the Democratic Republic of Congo won't be the same again as the opposition forces will likely spoil the party for him to the detriment of his war weary country.

Let us wait and see what will transpire.
 
Hii tabia ya kuonea wapinzani imeshika kasi sana kwenye huu ukanda wetu.
Cha ajabu huyu anaekamata wenzake na yeye alikuwa kama mpinzani juzi kati na Kabila akaamua kabisa kumpisha kitaarabu
Kwahiyo nina uhakina hata chadema wakishika nchi lazima wanyanyase wapinzani wengine ndio kawaida ya mtu mweusi
 
Mkoloni alianzisha Dola na mahakama na alivitumia Kwa ubabe wa kiwango Cha juu zaidi Cha ukatili kuzididimiza jamii za KIAFRIKA

HTM- KIDATO CHA PILI
 
Hii tabia ya kuonea wapinzani imeshika kasi sana kwenye huu ukanda wetu.

TShisekedi nayeye si alikuwa mpinzani juzi tu leo kaota mbawaa !!

Na michadema ikipatq nafasi ndio yatakuwa ivi kwa wapinzani wake!!
 
Chanzo cha haya yote ni CCM.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom