Uchaguzi 2020 Mshituko: Wananchi Kigoma mjini wamtaka Prof. Joyce Ndalichako

Uchaguzi 2020 Mshituko: Wananchi Kigoma mjini wamtaka Prof. Joyce Ndalichako

Mbona walimu wanalia kila kona kuhusu masilihai yao amewatetea kwa kiasi gani ?.Volume ya kazi ni kubwa anachoka kuhudumia wanafunzi zaidi ya uwezo wake.Wastaafu hawapati in time mafao yao,kupandishwa madalaja ni shida,Ajira ni taabu .Vitisho kwa walimu ni shida au shughuri za Jaffo yeye ndie anazibeba?
 
"OCD, put this man inside untill tomorrow". Prof. J. Ndali!.
 
Huyu Prof atatufaa sana Kigoma mjini, siyo msaliti kama Zito Kabwe wa kujipendekeza kwa mabeberu.
IMG_20200127_065105.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zitto wala hana wasiwasi na hilo kwani hata akigombea wete atapita tuu.
Kwa kweli kwa Wete atapita, ila kwa Kigoma Mjini inabidi tumuombee. Zitto anatia mpira kwapani, hatagombea ubunge kwa kuogopa kutafunwa kichwa na wapiga kura wenye hasira kali.
 
Kama wazee wanamtaka tunawashauri waende nyumbani kwake yupo tele watamkuta.
 
Elitwege,
Wanaomtaka Ndalichako ni wanaccm wenzako na siyo wananchi wa Kigoma kama unavyodai. Wananchi halisi wa Kigoma wanajitambua na hawawezi kuwa mawakala wa chama cha wabakaji wa demokrasia na haki za kiraia.
 
Tangu prof Ndalichako atangaze kugombea Jimbo la zitto, huyu dogo kaanza kuweweseka na kutupa maneno yasiyokuwa na maana akidhani atamharibia Prof. Anaona huu mkopo utamjenga kisiasa Prof hajui Sasa ndio atapita kiulaini kwani atawaahidi wamchague ili akashughulikie mkopo haraka awajengee shule.

Hili la watoto kwenda shule wanaonyonyesha Ni kituko tu Kama vya brazaK, sanasana linatoa taswira kuwa waafrica Ni wapuuzi. Prof Ndalichako komaa nae tu asikutishe mwache aandike barua Hadi kwa papa.
 
Kwa akili ya zitto anadhani kamkomoa magufuli. Sasa hao wenye mimba waliokosa hela ni wangapi na hao wasio na mimba waliokosa hela wangapi.? Unapoenda kuzungumzia masuala ya mimba kwenye dunia ya watu ambao wao watoto zao hawatarajii au sio utamaduni kupata mimba kizembe ni sawa na kusema

•huku kwetu watoto wa shule kupata mimba ni jambo la kawaida,

•ni janga la taifa,

•serikali imeshindwa na wazazi wameshindwa,

•kwamba wanaopata mimba ni wengi kuliko wasio na mimba.

•sawa atasema wanabakwa je ni kweli wengi wanabakwa au wanavua wenyewe chupi? Je nchi ina kiwango kikubwa cha wabakaji?

•tafsiri yake hata mama yake shuda salum (RIP)alisoma akiwa na mimba.

•lakini hata mama zetu tafsiri ni kuwa walisoma na mimba isipokuwa magufuli ndio kaharibu utaratibu wa watu kusoma na mimba.

Katika kitu kinachomkera kila mzazi ni binti yake kupata mimba akiwa shuleni. Wazazi wengi walitamani kifanyike kitu cha kuwatisha binti zao ili wasichezee shule. Hii iliwapa woga fulani na iliwaepusha pia na madhara mbalimbali. Hata wazazi wengi waliwakumbusha binti zao hatari ya kupata mimba kwa maana ya kupoteza shule.

Kuna mwandishi wa literature alisema mtu anayependa umaarufu akishindwa kupata umaarufu kwa mambo mazuri hufanya mambo mabaya kupata umaarufu.

Zitto alizoea madhaifu ya ccm kupatia umaarufu. Anzia ishu ya buzwagi. Sasa amekuwa akiibuka na hoja mara takwimu, mara CAG,mara ndege used lakini watu wameshampuuza. Anadhani kuzuia hela kamkomoa magufuli wakati hizo pesa zingewasaidia na wanakigoma waondokane na ujinga.

Alivyokuwa mjinga eti anavimba kifua akiamini kafanya jambo la maana. Kuna msemo unasema colonialists planted the seeds of their own destruction. Na ujuaji hupofusha maono. Ndicho anachovuna au atakachovuna huyu bwana.

Maisha aliyoishi enzi za jk hayatajirudia tena. Apambane tu apate pesa kwa njia halali kama watanzania wengine.
FB_IMG_1571555344098.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
eddy, Acha kusema uongo tuulize tuliopo kigoma mama Ndalichako amejiwekeza jimbo la Kasulu Mjini na watu wote kigoma wanajua ndio mgombea wa jimbo hilo. Kuhusu KIGOMA mjini walimuomba akagombee huko sababu alisomea huko na kuishi huko katika makuzi yake. Kasulu alikuwa hana nyumba lakini kajenga na haipiti miezi miwili bila kuja hapa Kasulu na ameboresha sana sekta ya elimu Kasulu. Hivyo sahau huyo mama kugombea KIGOMA , kesha jijenga Kasulu na waha wamemkubali hapa hana mpinzani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
eddy, Acha kusema uongo tuulize tuliopo kigoma mama Ndalichako amejiwekeza jimbo la Kasulu Mjini na watu wote kigoma wanajua ndio mgombea wa jimbo hilo. Kuhusu KIGOMA mjini walimuomba akagombee huko sababu alisomea huko na kuishi huko katika makuzi yake. Kasulu alikuwa hana nyumba lakini kajenga na haipiti miezi miwili bila kuja hapa Kasulu na ameboresha sana sekta ya elimu Kasulu. Hivyo sahau huyo mama kugombea KIGOMA , kesha jijenga Kasulu na waha wamemkubali hapa hana mpinzani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Zito lazima atupwe nje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom