BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemruhusu mshtakiwa Said Matwiko anayekabiliwa na kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine zenye uzito wa kilo 34.89 kuonana na mke wake Sarah Joseph ili wajadiliane kuhusu malezi ya watoto wao.
Sara na mume wake pamoja na watu wengine watatu akiwemo aliyekuwa kocha wa makipa wa timu ya Simba Sport Club, Muharami Sultan (40) wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya kinyume cha sheria.
Kuruhusiwa kwa wanandoa hao kuonana mahakamani hapo, kunatoka na ombi lililowasilishwa na Matwiko mahakamani hapo.
Machi 16, 2023, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.
Tofauti na siku nyingi ambapo washtakiwa husikilizwa kesi yao kwa njia ya video, leo Machi 30, 2023 , washtakiwa wote wameletwa Mahakama kwa ajili ya kusikiliza kesi yao.
Hata hivyo upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.
Pia soma: